Charles James, Michuzi TV
BAADA ya kupanda Ligi Kuu, Mabingwa wa Ligi daraja la kwanza, Dodoma FC wametamba kufanya usajili kabambe ili kuhakikisha wanafanya vizuri na kutoa ushindani kwa Timu zingine.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi leo alipokua akizungumza na Michuzi Blog ambapo ametamba kuifanya Dodoma FC kuwa miongoni mwa timu tishio zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara.
Kunambi amesema katika kuiandaa timu yao kufanya vizuri wameandaa bajeti ya Sh Milioni 500 kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji bora na wenye uzoefu wa Ligi.
Amefichua kua hata kiungo Waziri Junior ambaye amejiunga na Yanga walishafanya mazungumzo nae ya kumsajili lakini wakazidiwa na Yanga.
" Dodoma FC hatuna utani na suala la usajili, tumeandaa bajeti kubwa ya usajili wa wachezaji 11 kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi, na hiyo ni baada ya kuwaondoa wachezaji 15 hivyo lazima kusajili.
Kocha wetu Mbwana Makata tunaendelea nae kwa sababu kazi aliyofanya na benchi nzima la ufundi ni kubwa na hata maslahi tutawaboreshea, wamepambana kurudisha hadhi ya soka la Dodoma na hakika wameweka historia kubwa kwenye Jiji letu," Amesema Kunambi.
Amewataka wananchi wa Dodoma kuendelea kuiunga mkono Timu yao ili Waziri kufanya vizuri zaidi na kwamba wao kama Halmashauri ya Jiji watazidi kuweka mbele maslahi ya timu hiyo ili kuepuka kufanya vibaya.

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumzia usajili wa Timu ya Dodoma Jiji FC ambayo imepanda Daraja na sasa itacheza Ligi Kuu msimu ujao wa 2020/21.
Kikosi cha Timu ya Soka ya Dodoma Jiji FC ambayo imepanda Daraja na sasa itacheza Ligi Kuu msimu ujao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...