MGOMBEA  wa ubunge Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo jana amesimamisha Jiji la Arusha wakati akirejesha fomu ya kugombea ubunge huku  wananchi wakiwemo wanachama wa CCM na wasiokuwa wanachama Chama hicho wamejitokeza kwa wingi kumsindikiza mgombea huyo.

Aidha maeneo mbalimbali ya jimbo hilo wananchi wengi walijitokeza kumuunga mkono, huku wakimwambia asihofu kwani wameshajipanga kumpa kura yeye , madiwani pamoja na Rais  na kwamba kura watakazo piga kwa kipindi hiki zitakuwa za kihistoria.

Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu mgombea Jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM Gambo,  aliwashukuru wananchi na wanachama wa CCM kwa kumsindikiza   kurejesha fomu huku akiyaamini mapenzi  waliomuonesha.

Amebainisha awali miaka ya nyumba kabla ya Rais Magufuli kuingia madarakani watu walikuwa wanaogopa kuvaa  hata sare za CCM lakini kutokana na  kazi alizofanya  Rais wetu na zimekubalika ndio maana sasa hivi wanaweza kuvaa sare hizo na kupita sehemu yeyote Ile

Amesema iwapo tume itampitisha  atashirikiana nao pamoja na  viongozi   katika kila jambo  ili Kuhakikisha Chama chao kinapita pamoja na kuwaletea wananchi maendeleo

"Namshukuru Mungu kwa kunisimamia kila hatua maana anapo simama hakuna anaezuia, Mungu akiamua kitu hamna binadamu anaeweza kuzuia.Niwaombe mniombee mimi na Rais wetu,"amesema Gambo

Amesema kuwa alipokuwa njiani anaelekea kurejesha fomu alipokea ujumbe mfupi wa maneno uliotoka kwa mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA unaosema " Nilikuwa sijui kama wewe ni mjomba wangu ,na iwapo ningejua unapitishwa na Chama chako nisinge gombea .

"Mimi namtumia tu taarifa kuwa mama yangu alikuwa ni  mchaga  na nimwambie sio mamangu tu hata mke niliyemuoa ni mchaga, kwa hiyo yeye asihofu aje tukutane uwanjani tujue mbivu na mbichi, naniseme tu tukipitishwa naahidi kupiga kampeni za amani na utulivu,"amesema Gambo.

Ameongeza kuwa aao hawatapeleka majungu kwenye majukwaa bali wataenda  kuelezea shida za wananchi na kuwaambia namna ya kuzitatua.Amewataka wananchi kundelea kutunza kadi zao za kupiga kura ili ikifika Oktoba 28,2020 wajitokeze wakachague viongozi watakao waongoza vyema.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...