Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imesema tayari imeanza ujenzi wa barabara kiwango cha lami katika Mji wa Kiserikali Mtumba jijini Dodoma ambapo barabara zenye urefu wa km 11.2 zitakua za njia nne na barabara zenye urefu wa km 28 zitakua za njia mbili.

Barabara hizo zenye km 11.2 zitakua zikipitisha magari mawili kila upande wa barabara wakati zenye km 28 zitakua zinapitisha gari moja kila upande na hivyo urefu wa barabara zote jumla utakua ni km 51.2.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo wakati akisoma taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa kazi za miundombinu ya Wizara yake katika kipindi cha miaka mitano leo jijini Dodoma kwenye maadhimisho ya siku ya miundombinu.

Waziri Jafo amesema miundombinu mingine inayojengwa ni Makalvati makubwa 20, madogo 52, njia za watembea kwa miguu na baiskeli zenye upana wa mita 2.71 kila upande wa barabara, vituo vya kupakia na kushushia abiria, taa za barabarani 739, mifereji ya maji ambapo gharama za mradi huo jumla ni Sh Bilioni 89.13.

Kuhusu ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa fedha kutoka serikali kuu, Jafo amesema katika mwaka wa fedha 2019/20 Tamisemi iliidhinishwa fedha kiasi cha Sh Bilioni 33 kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizo kutoka mfuko mkuu wa Serikali ikiwa ni ahadi ya Rais Dk John Magufuli aliyoitoa mwaka 2015.

Miradi hiyo itakapokamilika itawezesha Makao Makuu ya Halmashauri na Miji Midogo kuwa na barabara za kiwango cha lami na kuboresha usafiri na usafirishaji pamoja na utoaji huduma za kiuchumi na kijamii.

Jafo amesema katika kipindi cha miaka mitano Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) limeshirikiana na Tamisemi katika kutekeleza mradi wa uondoaji wa vikwazo vya upitikaji wa barabara maeneo ya vijijini.

" Miradi hii imetekelezwa kupitia programu ya kuboresha barabara maeneo ya vijijini (IRAT) ambayo utekelezaji wake ulikamilika katika mwaka wa fedha 2018/19 ambapo mradi huo umetekelezwa katika Halmashauri 40 na jumla ya miradi iliyotekelezwa ni 55.

Kupitia IRAT tumeweza kufungua mtandao wa barabara wenye urefu wa km 2000 ambao ulikua haupitiki kutokana na vikwazo vya mito, mabonde na sasa mradi huu umenufaisha watu wapatao milioni tatu waishio vijijini ambao walikua na changamoto ya usafiri, " Amesema Jafo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumzia mafanikio ya Wizara yake kwenye miundombinu leo jijini Dodoma katika kilele cha wiki ya Tamisemi ambapo leo ilikua siku ya Miundombinu.
 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya Tamisemi ikiwa leo ilikua ni siku ya Miundombinu. Maadhimisho hayo yamefanyika kwa siku tatu jijini Dodoma.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akifuatilia mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo leo ikiwa ni kilele cha wiki ya Tamisemi.
 Wadau mbalimbali wa maendeleo wakifuatilia maadhimisho ya siku ya miundombinu ambapo Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo alikua akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa kazi za miundombinu ya Wizara yake katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...