Charles James, Michuzi TV

WANAFUNZI waliokua wakisoma China ambao serikali ilituma Ndege yake kwenda kuwafuata baada ya kutokea kwa mlipuko wa ugonjwa wa Covid19 (Corona) wamempongeza Rais Dk John Magufuli kwa moyo wake wa upendo kwa kuwajali.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi hao, Ahidi Sinene ambaye ni kiongozi wao amesema kama siyo moyo wa upendo wa Rais Magufuli pengine wangekwama kurudi nchini kutokana na gharama za usafiri kuwa juu baada ya kutokea kwa mlipuko huo.

Sinene amesema baada ya kuomba msaada kupitia kwa Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki serikali ilituma ndege yake aina ya Boeing 787 kuwafuata na kuwasafirisha moja kwa moja kwa gharama nafuu ambayo ni nusu ya bei ya mashirika mengine.

" Hakika moyo aliouonesha Rais wetu ni wa kipekee sana, kutuma ndege ya serikali Kuja China tena ikiwa tupu kwa ajili ya kutufuata sisi imetufanya tujione wa thamani kwenye Nchi yetu na kujivunia Rais wa namna hii.

Nauli ya kutoka China hadi huku ilikua zaidi ya Dola 2500 kwa mashirika mengine ya Ndege, tena hapo inakulazimu upite kwenye Nchi za hayo mashirika lakini Rais akatuma ndege ikaja tupu na bado ikatubeba kwa Dola 1200 ambayo ni nusu ya nauli ya ndege zingine tena tukaja moja kwa Moja nyumbani, tunamshukuru sana Rais wetu," Amesema Sinene.

Pia wamempongeza Rais Magufuli kwa namna alivyolitatua tatizo la Corona nchini bila kuzuia watu kuendelea na shughuli zao jambo ambalo Nchi zingine zimshindwa kwa kuzuia wananchi wao kutoka na kufanya maisha yawe magumu.

" Tazama wenzetu wanavyoteseka na 'lockdown' lakini sisi tuko mitaani tunafanya kazi zetu na Corona haipo, Rais alituondoa hofu na akasisitiza tuchukue tahadhari ikiwemo njia za asili na sote tumeona ilivyotusaidia," Amesema Sinene.

Sinene amesema kwa niaba ya wenzake 250 waliosafiri na ndege hiyo wanamshukuru pia Balozi Kairuki kwa kufanikisha safari yao hiyo huku akisema watanzania wana bahati ya kuwa na Rais kama Magufuli ambaye anajali utu wa wananchi wake.


Kiongozi wa wanafunzi waliokua wakisoma nchini China, Ahidi Sinene akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dodoma alipokua akimshukuru Rais Magufuli kwa kutuma ndege kuwachukua kipindi cha Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...