Na Khadija seif, Michuzi Tv
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Harrison Mwakyembe amezindua kuonyesha filamu za bongo kwenye nyumba za Sinema itasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. 

Akingumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam wakati  akizindua  sheria na kanuni za kuonyesha filamu kwenye majumba ya Sinema,  Mwakyembe amesema kuwa ni wakati wa kuendana na kasi ya sasa ya kiteknolojia pamoja na maendeleo. 

"Miaka 9 tumekua tukiendesha tasnia ya sanaa kwa kanuni za zamani za mwaka 2011, na kumekuwa na malalamiko ya wadau wa sanaa kuwa inatakiwa iendane na kasi ya sasa na kuachana na zamani. 

"Hivyo kwa sasa tunazindua kanuni mpya, zinazoendana na kasi ya sasa ya mwaka 2020, ili kuwasaidia wasanii kufanya kazi kwa uhuru, niwaombe wamiliki kutoa kipaumbele asilimia 60 kwa kazi za ndani na asilimia 40 kazi za nje"alisema Mwakyembe. 

Aidha aliongeza kuwa asilimia 80 wadau walikuwa wakitaka mabadiliko hivyo tumeondoa tozo ya kila mwaka kupitia filamu, Sasa hivi filamu ikitoka inahakikiwa mara moja tu kwa miaka yote.

Hata hivyo amewataka wadau wafilamu hasa vyombo vya habari ambao wanajukumu la kununua kazi za wasanii na kuzionyesha kutowakandamiza kwenye mikataba yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania, Profesa Frowin Ngoni alisema kuwa wamezindua kuonyesha filamu kwenye nyumba za Sinema ili watanzania wapate nafasi ya kuangalia filamu za zao. 

"Kuzinduliwa kwa kanuni hizi ikawe chachu na maboresho ya tasnia hi na tunategema kazi nyingi nzuri na zenye ubunifu kutokana kwa tozo hizi kupungua."

Kaimu Katibu Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Kiagho Kilonzo amesema kuwa wasanii wajitahidi kufanyakazi nzuri na kwa wingi ili kusaidia Uchumi wa nchi yetu.

"Malalamiko yalikua mengi na hiki Ni kilio kingine kilikua Kila simu wasanii wanalilia kuletewa kwa sheria hizo."

Pia amewaomba wasanii kutosita kukutana na viongozi wa bodi ya filamu na kuleta maoni pale ambapo watahisi itaweza saidia kukua kwa tasnia hii ikiwezekana hata kuikosoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...