Naibu waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba akipata maelekezo kutoka kwa mkulima wa zao la  Muhogo wakati akitembelea banda la  halmashauri ya wilaya ya Hanang Kateshi Mkoani Manyara katika maonesho ya 27 ya kilimo na sherehe za nanenane Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha.
 Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Omary Mgumba akipata maelekezo kutoka kwa mtaalam mwanafunzi wa dawa za asili za kuua wadudu katika mboga katika halmashauri ya jiji la Arusha kwenye maonesho ya 27 ya kilimo na sherehe za nanenane Themi Jijini Arusha.
Mhe.Omary Mgumba akipewa maelezo kutoka kwenye kituo cha mafunzo ya kilimo cha horticulture kwa vitendo katika maonesho ya 27 ya kilimo nanenane Them Jijjjj Arusha.
 Naibu waziri wa Kilimo Ommary Mgumba akiweka msisitizo kwa wakulima,wafugaji na wavuvi katika ufunguzi wa maonesho ya 27 ya kilimo na sherehe za nanenane yanayoendelea katika viwanja vya The,Njiri Jijini Arusha

Na,Jusline Marco;Arusha

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Ommary Mgumba amewataka wakulima,wafugaji na wavuvi kujiunga kwenye vyama vyao vya kisekta na ushirika ili serikali na sekta binafsi ziweze kuwafikia kwa urahisi na kuwapa huduma zao.

Akifungua rasmi maonesho ya 27 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini ambapo ameeleza kuwa kutokana na asilimia 75 ya wakulima kutegemea kilimo,Mifugo na uvuvi wanatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao yanayotokana na sekta hiyo kutokana na teknolojia zilizopo na hatimaye kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla.

Aidha amesema kuwa wafugaji,wakulima na wavuvi hawawezi kuondokana na umaskini kama hawatakuwa na ushirika imara utakao waunganisha kupata masoko na mikopo ili kuweza kuongeza kipato chao.

Vilevile ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 40 ya mazao inapotea baada ya mavuno hivyo kutokanana upotevu huo serikali imeamua kujenga vihengr na maghala ya mazao ya nafaka ili kuweza kuhifadhi mazao hao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Iddy Kimanta katika ufunguzi huo amesema kuwa maonesho hayo hayatakuwa na faida kama hayatabadilisha shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi zinazofanywa na wananchi.

Kimanta  amesema kuwa ili kuendeleza maonesho hayo mikoa yote mitatu ishirikiane katika kukusanya takwimu za wakulima, wafugaji na wavuvi walionufaika na teknolojia mbalimbali zilizopo katika maonesho hayo.

Awali akitoa taarifa fupi ya maonesho ya nanenane kwa mwaka 2020,Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto za covid 19 juhudi za uhamasishaji zilifanyika ambapo makundi 16 wamejitokeza kushiriki katika maonesho hayo.

Amesema kuwa wadau wamejikita katika kuonyesha mnyororo wa thamani wa kilimo na mifugo ambapo wanaendelea kuonyesha umahiri katika kuknyesha namna uzalishaji wa tija mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi pamoja na kuyasindika na kuifanya nchi kuingia katika uchumi wa kati.

 Ameongeza kuwa zipo changamoto ambazo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi ikiwemo uchelewaji wa wadau kujisajili hali iliyopelekea kutotambulika kwa washitiki ambao wameingi mwisho wa zoezi hilo.


Katika maonesho hayo pia Meneja wa kituo cha uwekezaji Tanzania Kanda ya Kaskazini Bw.Daudi Riganda amewataka wawekezaji nchini kulipa kodi za serikali mara baada wapatapo faida.

Riganda amesema kuwa kama ilivyo kaulimbiu ya maonesho ya mwaka huu kujikita zaidi kwenye Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Kituo hicho kimejitokeza kushiriki maonesho hayo kwa lengo la  kuhamadisha uwekezaji katika maeneo hayo ambapo Kanda ya kaskazini imejaliwa kuwa na utajiri wa kustawisha mazao ya nafaka kama mbigamboga ,maua na matunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...