Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Paradigm Initiative Afrika limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanasheria, waandishi wa habari na walimu na makundi mengine ya kijamii wamekutanishwa na kwa  ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao  ya kijamii kwa sasa na baadae.

Majadiliano hayo  yamehusisha  nchi za Afrika ya Kati ikiwemo Nigeria ambapo wadau wa mitandao kutoka katika nchi hiyo walishiriki kikamilifu pamoja na kutoa maoni yao kwa njia ya mtandao  walitamani kupata uzoefu kutoka Tanzania ambayo tayari imepiga hatua ikiwemo kudhibiti kikamilifu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Pamoja na mambo mengine wadau wamepata nafasi ya kuangalia na kujadili muswada wa Nigeria unaohusu masuala ya matumizi ya mtandao pamoja na kuangalia ni maeneo gani ya kusaidia kuboresha ufanisi pamoja na misingi bora ya utumiaji ya mitandao ya kijamii kwa Tanzania na Afrika ya sasa kwa siku za baadae.

Akizungumza kuhusu majadiliano hayo Mdau na mtumiaji wa mtandao,Mratibu wa majadiliano hayo, Peter Mmbando amesema kwamba ni wakati mwakafa wa kubadilishana uzoefu kati ya Tanzania na nchi nyingine ili kuona nini cha kujifunza kuendana na wakati kwa mahitaji ya sasa na baadae.

"Nawahisi watumiaji wa mtandao tuendelee kufuata sheria zilizopo ili kuendana na mahitaji ya sasa lakini kama kutakuwa na maboresho tufikishe maoni yetu kwenye vyombo husika kwa ajili ya kujadili na kujenga hoja," amesema

Ameongeza washiriki wametoa maoni yao kulingana na muktadha wa nchi yetu na nchi nyingine za Afrika kama bara moja ambalo linatamani kuwa na maudhui yanayoendana na Waafrika katika kutumia intanenti.



 Mratibu wa masuala ya kimtandao kutoka Shirika la Paradigm Initiative, Peter Mmbando (kushoto) akijadiliana jambo na wanasheria waliokuwa wakishiriki majadiliano yaliyohusu sheria ya matumizi ya mtandao pamoja na kujadili haki za mtumiaji kuendana na uhitaji wa matumizi ya sasa na baadaye, yaliyofanyika Dar es Salaam jana.
 Baadhi ya Wanasheria na washiriki wengine wakijadiliana jambo kuhusu sheria ya matumizi sahihi ya mtandao pamoja na kujadili haki za mtumiaji kuendana na uhitaji wa matumizi ya sasa na baadaye.
 Mmoja wa wadau wa masuala ya mtandao akiandika maelezo wa majadiliano yaliyowakutanisha wadau mbalimbali waliokuwa wakijadili matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa kuangalia sheria zilizopo
 Wanasheria wakiwa makini kusikiliza maelezo ya mmoja ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kutoka nchini Nigeria aliyeshiriki majadiliano hayo kwa njia ya mtandao yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
 Mshiriki Samuel Mbilinyi (kushoto) akiwa makini kumsikiliza mmoja ya washiriki kutoka nchini Nigeria.Katikati ni Elizabeth James pamoja na Catherine Ngoge wakifuatilia majadiliano hayo.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari wakiwa na mdau wa matumizi sahihi ya Intanenti Peter Mmbado( wa pili kulia)wakifurahia jambo wakati wa kikao hicho cha majadiliano
 Mmoja ya washiriki Maria Mrindoko akifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea kwa njia ya mtandao kuhusu masuala mbalimbali ya sheria za matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii
 Waandishi wa habari Zainabu Nuru wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea
Sehemu ya washiriki wakiwa makini kuangalia masuala ya sheria ya mtandao wakiendelea na kuangalia vipengele ikiwa ni sehemu ya kuendelea kubadilisha uzoefu    kati yao na wadau wengine wa nchi za Afrika ikiwemo Nigeria
Wadau mbalimbali wa masuala ya utumiaji wa mitandao ya kijamii wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa majadiliano yaliyowakutanisha wadau hao kuangalia matumizi sahihi ya mitandao kwa kuangalia sheria zilizopo kwa nchi za Afrika
Mshiriki Ibrahim Haule akiandika jambo wakati wa majadiliano hayo yakiendelea
Wadau wakiendelea na majadiliano kuhusu matumizi sahihi ya mtandao kulingana na sheria ya mtandao nchini na kupata uzoefu wa nchi nyingine za Afrika walioshiriki kwa njia ya mtandao
Washiriki wakiendelea kuchukua maelezo wakati wa majadiliano hayo yakiendelea .(PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...