Napenda
kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Dkt. John Pombe Magufuli
kuchukua fomu ya kugombea urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
ninamtakia kila la heri airejeshe tayari kwa ushindi Octoba 28, 2020.
Nasema
ushindi kwa maana kati ya wote tuliosikia wanagombea hakuna anayefikia
hata robo ya uzalendo, uadilifu, uchapa kazi, ufuatiliaji na ucha Mungu
alio nao Dkt. Magufuli ambao umetuvusha miaka mitano mpaka sasa tupo
kwenye uchumi wa kati.
Dk.
Magufuli ndio tumaini na tegemeo la pekee la Mtanzania mnyonge na
maskini kwani amewawezesha kusoma bure shule ya Msingi hadi sekondari,
amewajengea hospitali, vituo vya afya, Zahanati kila kona ya nchi na
kuwaweka Madaktari, Madawa na vifaa tiba.
Ni
Dkt. Magufuli huyu huyu ametupatia heshima Watanzania kwa kuhakikisha
tunanunua ndege zetu wenyewe; tunajenga reli ya kisasa ya umeme ya SGR;
tunajenga Bwawa kubwa la umeme utakaozalisha megawatts 2115; amejenga
Miundombinu ya kisasa ya Madaraja, barabara, viwanja vya ndege na
amehakikisha rasilimali zetu zinatunufaisha sisi Watanzania kuliko
kipindi chochote kile.
Alipoona
Wakulima wanaonewa aliingilia kati bei za mazao; Amehakikisha huduma
kwenye ofisi za umma zinaimarika na leo hii hakuna tena matabaka wala
uonevu wa Wenye nguvu kwa Wanyonge. Tumpate wapi tena kama Dk. Magufuli?
Tulianza
na Mungu, tutamaliza na Mungu. Tumpe tena Rais Magufuli miaka mitano
akakamilishe miradi ya ujenzi mIkubwa aliyoianza; Kama aliweza
kutufikisha uchumi wa kati kwa muda wa miaka 5 tu, hadi 2025 nchi yetu
ya Tanzania itakuwa kama Ulaya mpya. Itakuwa ni miaka 5 ya fursa,
maendeleo, raha zaidi na utajiri kwani misingi imara na mizuri
imeshawekwa.
- Emmanuel J. Shilatu
DO MIHAMBWE
0767488622
Mgombea wa Urais Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ilani ya Uchaguzi wakati
akiongea na wanachama wa CCM wa Dodoma baada ya kutoka kuchukua fomu
hizo za kugombea Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma
akiongea na wanachama wa CCM wa Dodoma baada ya kutoka kuchukua fomu
hizo za kugombea Urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...