Na Amiri Kilagalila,Njombe
Bweni
moja la wasichana wa shule ya Sekondari Maguvani halmashauri ya Mji wa
Makambako mkoani NJOMBE limenusurika kuungua moto usiku wa tarehe 20
majira ya saa mbili usiku.
Mkuu wa shule hiyo
TUDEN MAHENGE amesema tukio hilo ni la Tatu huku likiungua mara mbili na
sababu zikidaiwa ni wananchi ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya eneo
hilo kujengwa shule.
Akiwa ameambatana na
kamati ya Ulinzi na usalama Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Mhandisi MARWA
RUBIRYA amekuatana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Makambako PAUL
MALALA ili kupata taarifa ya awali.
"Mimi
nikiwepo hapa halmashauri ya mji ya Makambako hii ni mara ya pili,mara
ya kwanza vile vilev ilitokea bweni lile lile na tuna takribani mwaka
mmoja tangu tumalize ukarabati"alisema Paul Malala
Baada
ya kuwasili katika shule ya Sekondari MAGUVANI kamati hiyo imekagua na
kushuhudia uharibifu wa samani za bweni na mali za wanafunzi.Mkuu wa shule hiyo TUDEN MAHENGEMwalim Mahenge amesema tukio hilo ni la Tatu kutokea.
"Moto
wa kwanza ulitokea machi 2018 na uliunguza jengo zima la
wasichana,lakini 2018 mwezi septemba uliwaka tena kwa kuanzia juu ya
kitanda cha msichana mmoja ukateketeza vitanda vitatu vya wanafunzi na
godoro tatu.Na ndio hisia za moto huu awamu ya tatu uliotokea tarehe 20
saa mbili usiku wakati wanafunzi wako kwenye maandalizi ya
kujisomea"alisema
Na ndipo Mkuu wa mkoa wa
NJOMBE Mhandisi MARWA RUBIRYA akavitaka vyombo vya ulinzi na usalama vya
mkoa huo kuhakikisha wanakomesha vitendo hivyo.
"Nimeshatoa
maelekezo kwa kamanda wa polisi wa mkoa wafanye upelelzi wa kina
kuhakikisha wote waliohusika wanakamatwa na wanafikishwa kwenye vyombo
vy sheria"alisema Rubirya
Kamanda wa Polisi mkoa
huo HAMIS ISSAH ameshauri wakuu wa shule kuandaa utaratibu wa kujilinda
huku jeshi hilo likitoa msaada wa doria wakati wa usiku.
Katika
ajali hiyo vitanda viwili vimeungua na vitu kadhaa vya wanafunzi
vikiwemo madaftari magodoro mablanketi na viatu vimeungua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...