Na Piason Kayanda, Michuzi TV

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili, Rose Muhando rasmi amethibitisha kushiriki katika tamasha lililoandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion maalumu kwa ajili ya kuombea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Rose Muhando amesema amejipanga vyema kuelekea tamasha hilo na kusema kuwa waimbaji wote wamejipanga kutoa burudani ya kutosha katika tamasha hilo.

 "Waimbaji wote tumejipanga vizuri viongozi ni wa kwetu kila muimbaji anajua kwa nini yuko pale".

Waimbaji wengine watakao tumbuiza katika tamasha hilo ni Christina Shusho, Boniphace Mwaitege na Upendo Nkone na wegine wengi.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amesema tamasha hilo lililo tarajiwa kufanyika August 23, mwaka huu limehamishiwa na litafanyika Septemba 6 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na kiingilio kitakuwa bure.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...