TAASISI
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Simanjiro Mkoani
Manyara, inawashikilia madereva watatu wa malori wakidaiwa kukwepa
ushuru wa mazao .
Mkuu
wa TAKUKURU mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini
Babati Agosti 13 amesema madereva hao walishirikiana na baadhi ya
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kukwepa ushuru.
Anasema madereva hao walitumia magari aina ya malori yenye namba za usajili T450 AZP, KCM 411 L na KCU 073 X.
Amesema madereva hao walishirikiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo Peter Sanga na Joachim Soka kukwepa ushuru huo.
Amesema
awali walipata taarifa ikiwatuhumu watumishi wa Halmashauri hiyo Sanga
na Soka kwa kuhusika na kuhujumu mapato ya halmashauri kwa kutoa risiti
za POS zinazoonyesha idadi ambayo ni nusu ya magunia ya vitunguu
yanayokuwa yanasafirishwa na malori.
"Hivyo
fedha za ushuru wa mazao ya magunia yanayozidi kwenye magari huingia
mifukoni mwao badala ya kufikishwa sehemu husika," amesema Makungu.
Amesema
kutokana na taarifa hiyo TAKUKURU kwa kushirikiana na polisi waliweka
mtego uliowezeshwa kukamatwa kwa malori matatu yakiwa na shehena kubwa
ya magunia ya vitunguu.
Amesema
stakabadhi za mashine ya EFD zilionyesha kuwa wamelipia serikalini
ushuru kidogo ukilinganisha na magunia ya vitunguu yaliyomo kwenye
malori hayo.
Amesema
watuhumiwa hao ambao ni madereva wa malori na mtumishi wa halmashauri
hiyo Soka wanashikiliwa na TAKUKURU kwa uchunguzi zaidi wa makosa ya
kula njama na kuisababishia hasara halmashauri ya wilaya.
"Jaji
mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma aliwahi kusema wakati
akifungua kongamano la wadau wa mapambano dhidi ya rushwa katika
mapambano dhidi ya rushwa katika mfumo wa utoaji haki Juni 17 mwaka huu
kuwa utashi wa kisiasa na dhamira anayoonyesha Rais Magufuli hsitoshi
bila ya kila taasisi, kila idara na kila halmashauri kukubali kwa
vitendo kuwa sehemu ya vita dhidi ya rushwa," amesema Makungu.
Amesema
taarifa za kufikishwa kwao mahakamani hupelekwa kwa uongozi wa
Halmashauri hiyo ambapo tofauti na Halmashauri nyingine za mkoa huo
huwasimamisha kazi mara moja kwenye halmashauri hiyo wanaendelea na
kazi.
"Kwa msingi huo ni
vigumu kupambana na rushwa ndani ya Halmashauri hiyo hadi pale viongozi
watakapokubali kwa vitendo kwa vitendo kuwa sehemu ya kupambana na
rushwa kuwasimamisha kazi.
"Ni
rai yetu kwa viongozi wa Halmashauri hiyo wakaunga mkono utashi wa
kisiasa na dhamira abayoonyesha Rais John Magufuli katika kupambana na
rushwa ili kubadilisha mitazamo ya baadhi ya watumishi wanaona hakuna
hatua madhubuti zinazochukuliwa na mwajiri dhidi yao hata wanapofikishwa
mahakamani kwa rushwa," amesema Makungu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...