Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akipewa
maelezo na Mkuu wa Idara ya Shule Huria na Elimu kwa Umma juu ya miradi
mbalimbali inayotekelezwa na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
alipotembelea Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam 19.08.2020. Kulia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima
Dkt. Naomi Katunzi (picha na TEWW)
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako (katikati),
Mwenyekiti wa Baraza la Usimamizi TEWW Dkt. Naomi Katunzi (Kulia kwake),
Mkurugenzi wa TEWW Dkt. Michael Ng’umbi (kushoto kwake) akiwa katika
picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Usimamizi la TEWW pamoja na
Menejimenti ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima baada ya kumaliza ziara
ya kutembelea taasisi hiyo jana 19.08.2020 jijini Dar es Salaam.
*********************************
Na Mwandishi Wetu- TEWW
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Taasisi ya Elimu ya
Watu Wazima (TEWW) kuhakikisha inatelekeza ipasavyo Mradi wa Kuinua
Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa kuwa TEWW moja ya Taasisi
inayotekeleza mradi huo.
Waziri Ndalichako ametoa
maagizo hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na
Wajumbe wa Baraza la Usimamizi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Amesema ni vizuri mradi huo
ukatekelezwa ipasavyo ili malengo ya mradi yaweze kufikiwa ambapo moja
kati ya malengo hayo ni kuwezesha mtoto wa kitanzania kuendelea kupata
elimu bora.
Aidha, Prof. Ndalichako
amesisitiza TEWW kuendelea kufanya kazi ninazoendana na dhima wa
uanzishwaji wa Taasisi hiyo ikiwepo utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa ya
Kisomo maarufu kama ‘NALMES’ pamoja na kuandika maandiko kwa ajili ya
miradi mingine kwa ajili ya kuwawezesha watanzania.
Katika hatua nyingine, Waziri
Ndalichako amepongeza Baraza la Usimamizi wa TEWW kwa kufanya majukumu
yake kwa ufanisi mkubwa toka ilivyozinduliwa mnamo Agosti, 2018.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu
ya Watu Wazima (TEWW), Dkt. Michael Ng’umbi amemwakikishia Waziri kuwa
TEWW itatekeleza mkakati wa Kisomo wa Kitaifa (NALMES) na ule wa SEQUIP
kama ambavyo ilivyokusudiwa kwa ajili ya maslahi mapana ya Tanzania.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...