Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kinondoni Anna Luvanda, akizungumza na  Kamati za ushindi za   CCM Kata ya Makongo ka upande wa  umoja huo, Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa UWT wa Wilaya hiyo Zahara Abdallah na kushoto ni Mwenyekiti wa UWT  wa Kata ya Makongo Juu na Mgombea Udiuwani Viti Maalumu, Janeth Mahawanga.
 
Mmoja na wanachana wa UWT Kata ya Makongo, akichangia mada katika kikao hicho.
Wanachama wa UWT  wakicheza muziki baada ya kumaliza kikao hicho cha kimkakati.



Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

UMOJA wa Wanawake Tanzania (UWT), wilayani Kinondoni,  jijini Dar es Salaam umeanza mikakati ya kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata ushindi mnono katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu .

Akizungumza katika mkutano wa ndani  wa Kamati za ushindi za  UWT , Kata ya Makongo Juu, wilayani humo, leo, Mwenyekiti wa jumuia hiyo wa Wilaya ya Kinondoni, Anna Luvanda, amesema wanawake ni jeshi kubwa linalotegemewa na Cha kupata ushindi, hivyo kuhimiza wanawake kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura.

Ameongeza hakuna ubishi kuwa Mgombea Urais wa CCM Rais Dk. John Magufuli  atashinda kwa kishindo ambapo pia nguvu kubwa  ni kuona madiwani na nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kawe  inarudi mikoni mwa CCM.

“Haiwezekani tukatawaliwa na Halima Mdee kwa miaka 15. Inatosha. Wanawake tusimame imara kuhakikisha mgombea wetu wa Ubunge, Askofu Josephat Gwajima inaibuka mshindi  Kawe. Changamoto ni nyingi hapa, zinazotokana na usaliti uliofanywa na wenzetu mwaka 2015,”amesema  Luvanda.

Amewataka wale wote ambao  walitangaza nia na kura zao kuto kutosha, wasilete nongwa  badala yake waungane  kuunda timu za ushindi kwani CCM mbele mtu baadaye.

Kwa upande wake Katibu wa UWT wa Wilaya ya Kinondoni Zahara Abdallah,  amesema muda wa kumng’oa Mdee jimbo la Kawe umefika  na awamu hii ni lazima ang’oke kutokana na kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa UWT wa Kata ya Makongo Juu  ambaye pia ni  mshindi wa nafasi ya Ubunge, Vitimaalumu, Janeth Mahawanga, amesema, Kata yake inakabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na kukosa mwakilishi na mtetezi wa wanawake, hivyo kuna kila sababu ya wanawake kuungana na kumng’oa  Mdee ambaye ameshindwa kutetea wanawake.

Mwisho..

CAPTION

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...