Kamishna wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma, Harold Nsekela akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa kata za kanda na makao makuu jijini Dar es Salaam leo.
 Kamishna wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma, Harold Nsekela akizungumza na watendaji wa kanda na makao makuu leo wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma, Harold Nsekela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua mafunzo ya watendaji wa Kata wa kanda pamoja na makao makuu.

 CHANGAMOTO kubwa hapa nchini kwa viongozi ni Mgongano wa Maslahi katika uongozi hivyo Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma ikishirikiana na Uongozi wa shule ya Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imeandaa mafunzo kwa watendaji wa kanda zote nchini pamoja na makao makao makuu ili kutoa mafunzo ili kuepukana Mgongano wa maslahi wakati wa utumishi wao.

Kamishna wa maadili kutoka Ofisi ya Rais Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa Umma, Harold Nsekela akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akifungua mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo ya Mgongano wa maslahi katika uongozi yatawasaidia katika viongozikuwasiliana na katika vipindi mbalimbali kwenye vyombo vya habari.

Amesema kuwahuwezi kuhoji kuwa kiongozi kakosea wakati hujatoa elimu ya maadili kwa viongozi.

"Tumeamua kutoa elimu kwa vijana wawili wawili kwa kila kanda na makao makuu ili wapewe mafunzo ya Mgongano wa maslahi katika uongozi kwaajili ya kwenda kuzungumza na viongozi katika kanda zao." Amesema Nsekela.

Hata hivyo Nsekela amesema kwa kuzingatia sheria hasa kifungu cha nne na tano vimefafanua vizuri juu ya suala la mgongano wa maslahi ndio maana ya sekretarieti ya maadili imeandaa  sheria na kanuni zinazohusu udhibiti wa mgongano wa maslahi kwa viongozi.

Mafunzo hayo amesema yanahusu kuongeza uelewa juu ya dhana ya mawasiliano na uwasilishaji wa mada kuhusu mgongano wa maslahi, kuimarisha njia ya mbinu na mikakati ya mawasiliano kupitia vyombo vya habari na uwasilishwaji wa mada katika maeneo ya mgongano wa maslahi, kuongeza uzoefu na stadi za mawasiliano na uwasilishajo wa mada pamoja na kuhakikisha ujumbe unaotolewa kuhusu mgongano wa maslahi kwa viongozi wa umma na wananchi unawafikia kwa ukamilifu.

Nsekela amesema kuwa kukosa umahili katika kuzungumza au kuwasilisha vizuri mada kunaweza kukosesha heshima na kuaminika kwa taasisi na kutoeleweka kwa ujumbe unaokusudiwa kuwasuilishwa.

"Ukamilifu wa mawasiliano unatimia pale ambapo wapokeaji wa ujumbe husika wanaelewa ni nini muwasilishaji alikuwa anakusudia." Amesema Nsekela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...