Na Amiri Kilagalila,Njombe

Kanisa la Romani Katoliki parokia ya Utalingolo jimbo la Njombe mbioni kupata gari ya usafiri kwa ajili ya parokia kutokana na kukusanya Shilingi milioni hamsini na nne,laki tisa na arobaini na moja elfu,na mia nne hamsini (54,941,450/=) kutoka kwa wadau mbali mbali na harambee  iliyofanyika mapema August 2/2020 katika kanisa hilo.

Awali akitoa taarifa ya Parokia kwa niaba ya kamati ya harambee ya ukusanyaji wa fedha za ununuzi wa gari Ndug,Deo Mtewele amesema Parokia yenye vigango vinne vya Utalingolo,Igoma,Iliwa na Luhuji ilianzishwa rasmi mwaka 2011,lakini kumekuwa na shida ya utoaji wa huduma kutokana na kukosa usafiri huku ikilazimu kutumia njia mbali mbali ikiwemo kuazima kwa wadau

“Licha ya Changamoto ya usafiri lakini Parokia yetu imefanikiwa kufanya shughuli mbali mbali za kitume,pamoja na mafanikio moja ya changamoto yetu ni ukosefu wa gari ya Parokia kama chombo cha kurahisisha huduma mbali mbali za Kichungaji”alisema Deo Mtewele

Daktari Tobias Lingalangala ni mgeni wa heshima katika harambee ya ununuzi wa gari ilyofanyika katika kanisa hilo,kutokana na kuona changamoto za kanisa ameweza kuchangia shilingi Milioni 15 na kulitaka kanisa kutafuta gari mapema inayoweza kuendana na fedha iliyopatikana kuliko kusubiri kutafuta Milioni 100 ya makadilio na mahitaji yalio kuwa yamepangwa na kamati.

“Mtafute gari ambayo itakuwa nzuri na kwa hizi fedha mlizokusanya mkishirikiana na mimi kwa utulivu na kwa kuamini tunaweza kununua gari nzuri sana,kwa fedha hizi inawezekana” Alisema Dkt,Thobias Lingalangala Mgeni wa heshima harambee ya ununuzi wa gari ya Parokia ya Utalingolo,jimbo la Njombe.

Mwenyekiti wa kamati ya harambee Ndugu,Erasto Mpete amesema hawakuweza kutajia kupata kiasi hicho cha fedha kwa kuwa sio kitu kidogo kwao.

“Tukiongeza na kitita cha Mgeni rasmi kwenye fedha tulizokusanya jumla yake inatufanya kuwa na jumla ya milioni hamsini na nne laki tisa na arobaini na moja mia nne hamsini,kwa maneno mengine wanaparokia ya Utalingolo tumechanganyikiwa,kwa kweli tunamshukuru sana mgeni rasmi”alisema Erasto Mpete

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamesema hatua waliyofikia ni jambo la kushukuru Mungu kwa kuwa wanaamini Parokia yao sasa kupata usafiri kwa ajili ya Paroko utakaomuwezesha kufika sehemu yoyote kwa wakati.
 Ndugu Erasto Mpete mwenyekiti wa kamati ya harambee ya uchangiaji wa gari ya parokia ya Utalingolo akiwaonyesha wana parokia kitita cha fedha Milioni 15 iliyochangwa na mgeni rasmi Ndugu Tobias Lingalangala katika harambee ya uchangiaji wa fedha za ununuzi wa gari.

 Daktari Tobias Lingalangala na Mkewe wakiwa na waumini wa kanisa Katoriki kabla ya kuingia katika ukumbi ulioandaliwa kwa ajili ya harambee ya ununuzi wa gari ya parokia.
 Daktari Tobias Lingalangala akizungumza na waumini wa kanisa la Romani  Katoliki Parokia ya Utalingolo mara baada ya kukabidhi mchango wake utakaoongeza katika fedha ya ununuzi wa gari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...