Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mfano wa gunia la mahindi wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mfano wa gunia la mahindi wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa akitoa maelezo ya kuhusu uhifadhi wa nafaka mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA ametoa leo tarehe 8 Agosti 2020 kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu.

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa amepongeza ujenzi wa maghala na vihenge vya kisasa Mradi unaotekelezwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Waziri Mkuu ametoa pongezi hizo leo tarehe 8 Agosti 2020 wakati alipotembelea Banda la NFRA kabla ya kuhitimisha maadhimisho ya sherehe za wakulima Nanenane katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 
Waziri Mkuu amesema kuwa ujenzi huo ni mahususi kwa ajili ya Kuongeza Uwezo wa Kuhifadhi Nafaka kutoka tani 251,000 hadi tani 501,000. 

Akitoa taarifa ya Mradi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA Ndg Milton Lupa amesema Mradi huo unajumuisha ujenzi wa vihenge 56 na maghala ya kisasa 9 ambavyo kwa pamoja vinaongeza uwezo wa kuhifadhi kwa tani 250,000. Kwa sasa Mradi huu umefikia umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Amesema Uhifadhi wa nafaka kwa kutumia maghala ya kawaida, akiba inaweza kuhifadhiwa kwa takriban miaka mitatu tu kabla ya kuanza kupoteza ubora. Kwa kutumia vihenge vya kisasa, akiba inaweza kuhifadhiwa hata kwa zaidi ya miaka mitano bila kupoteza kiwango cha ubora.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni Taasisi ya Umma chini ya Wizara ya Kilimo iliyoanzishwa chini ya Sheria za Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 na kuanza kazi rasmi tarehe 1 Julai, 2008.

NFRA ina jukumu kuu la kuhakikisha usalama wa chakula ndani ya nchi kwa kununua, kuhifadhi na kutoa chakula katika maeneo yenye upungufu na kwa waathirika wa majanga mbalimbali.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...