Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye chumba cha nahodha wa meli
ya MV New Victoria – Hapa kazi Tu wakati alipokagua meli hiyo ambayo
ukarabari wake umekamilika kwenye Bandari ya Mwanza South, Agosti 9,
2020.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa nahodha wa meli ya MV New Victoria – Hapa Kazi Tu, Bembele Samson Ng’wita (wa pili kulia) wakati alipoikagua meli hiyo ambayo ukarabati wake umekamilika, kwenye Bandari ya Mwanza South, Agosti 9, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na nahodha wa meli ya MV New
Victoria – Hapa Kazi Tu, Bembele Samson Ng’wita kukagua meli hilo
ambayo ukarabati wake umekamilika , kwenye Bandari ya Mwanza South,
Agosti 9, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamlilo (wa tatu
kushoto) kukagua ujenzi wa meli mpya inayojulikana kama MV Mwanza - Hapa
Kazi Tu ,inayojengwa na Serikali kwenye Bandari ya Mwanza South ,
Agosti 9, 2020. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
==== ====== ====== =======
==== ====== ====== =======
WAZIRI MKUU AKAGUA UKARABATI WA MV NEW VICTORIA
*Aitaka mamlaka inayosimamia ihakikishe kuwa wiki
ijayo meli inaanza kazi
WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa amekagua ukarabati mkubwa
wa meli ya MV New Victoria Hapa Kazi tu na kuagiza mamlaka inayosimamia
ihakikishe kuwa kuanzia wiki ijayo meli hiyo inaanza kazi ya kusafirisha abiria
na mizigo kwa kuwa ukarabati umekamilika na sasa inaendelea kukaa tu hali ambayo ni hasara kwa Serikali.
Pia,
Waziri
Mkuu ametoa siku mbili kwa mamlaka inayohusika na utoaji wa kibali cha
kuanza
kazi kwa meli hiyo ihakikishe inatoa kibali hicho haraka na ratiba ya
safari itangazwe kwa sababu Watanzania wanahamu ya kuanza kuhuduiwa na
meli hiyo.
Waziri Mkuu ametoa
maagizo hayo leo (Jumapili, Agosti 9, 2020) baada ya kukagua meli hiyo ambayo
tayari imeshafanya safari ya majaribio kwa kusafirisha
abiria kutoka Mwanza hadi Bukoba mkoani
Kagera ambako ilirudi na abiria na mizigo.
Maeneo
aliyokagua kwenye meli hiyo ni pamoja na vyumba vya abiria vikiwemo vyumba
maalumu kwa ajili ya huduma za mama na mtoto, chumba cha kuongozea meli, vyumba
vya migahawa na chumba cha injini.
“Nimeona
ukarabati mkubwa uliofanywa, nimeona injini mpya, meli imekamilika na
ilishafanyiwa majaribio ya aina zote kubeba abiria na kubeba mizigo na
wataalamu wamejiridhisha kuwa inauwezo wa kubeba abiria na mizigo.”
Waziri Mkuu
ameongeza kuwa “Haya yote ni mawazo na mipango ya Rais Dkt. John Magufuli
pamoja na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015-2020.
Tumetekeleza na tunaendelea kutekeleza.”
Baada ya
kukagua meli ya MV New Victoria Hapa Kazi Tu, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa
chelezo pamoja na meli mpya na alieleza kuwa ameridhishwa na kazi inayoendelea
kufanyika na amewataka Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
Awali, Meneja
Miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Luteni
Kanali Vitus Mapunda alisema miradi hiyo minne ya ukarabati mkubwa wa meli ya
Mv Victoria Hapa Kazi Tu, MV Butiama Hapa Kazi Tu, ujenzi wa chelezo na ujenzi
wa meli mpya inayojulikana kama MV Mwanza Hapa Kazi Tu itagharimu sh.
152,916,249,842.
Alisema
ukarabati wa meli ya MV New Victoria Hapa Kazi Tu yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200
na mizigo tano 400 umegharimu sh. 22,712,098,200. Meli hiyo itatoa huduma ya
usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya bandari ya Mwanza Kaskazini, Kemendo
na Bukoba.
“MV Butiama itakayobeba
abiria 200 na mizigo tani 100 ukarabati wake umegharimu sh. 4,897,640,000. Meli
hiyo itatoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo kati ya bandari ya
Mwanza Kaskazini na Nansio Ukerewe. Ukarabati wa chelezo umegharimu sh.
36,152,511,642 na ujenzi wa meli mpya utagharimu sh. 89,154,000,000.”
Alisema
kukamilika kwa miradi hiyo ya kimkakati kutafungua fursa nyingi za ajira
binafsi na kupunguza gharama za usafirishaji sambamba na kuongeza tija katika
shughuli za biashara hivyo kuwafanya wananchi wanyonge wengi kunufaika. Ujenzi
wa Meli mpya unatarajiwa kukamilika Agosti 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...