AFISA Habari Msaidizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dominic Mgaya (37) na Mwanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE), Isaya Massawe (22) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na tuhuma za kusambaza maadhui mtandaoni bila ya kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Washtakiwa hao, wamesomewa mashtaka leo Septemba 18, 2020 mbele ya mahakimu wawili tofauti.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali,Adolph Ulaya Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Richard Kabate imedai kuwa, katika tarehe tofauti kati ya Oktoba 14, 2017 na Septemba Mosi, 2020 ndani ya jijini Dar es Salaam mshitakiwa, Mgaya alirusha maudhui hayo kupitia chaneli ya Youtube iitwayo Chadema Media Tv bila kuwa na leseni kutoka TCRA.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda makosa hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. 500,000 kila mmoja.

Mgaya ameweza kutimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana na kesi itatajwa tena Oktoba 20, 2020. 

Aidha mshtakiwa Massawe amefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Ruboroga na kudaiwa kuwa kati ya Februari 4, 2019 na Septemba 16, 2020 maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam, Massawe, alichapisha maudhui mtandaoni kupitia channel ya YouTube yenye jina la Isaya Thomas Massawe, bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Mshtakiwa Massawe amekana kutenda kosa hilo na kuachiwa kwa dhamana kufuatia kutimiza masharti yaliyomtaka kuwa wadhamini wawili waaminifu watakaosaini bondi ya Sh. milioni 3 kwa kila mmoja.

Hata hivyo, mshitakiwa ametimiza masharti hayo ya dhamana na kesi itatajwa Oktoba 15, mwaka huu. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Ofisa habari Msaidizi wa Chadema Dominic Mgaya akiwa katika ukumbi wa wazi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri kusomewa kesi yake ya kusambaza maudhui mtandaoni bila ya kibali.
Mwanafunzi wa chuoncha biashara CBE, Isaya Massawe akipelekwa mahakamani kwenda kusomewa kesi yake inayomkabili ya kusambaza maudhui mtandaoni bila ya kibali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...