AZAM FC KUMENYENA NA COASTAL UNION CHAMAZI KESHO.
Na Agness Francis,Michuzi Tv.
Na Agness Francis, Michuzi Tv.
KIKOSI cha Azam fc kesho kinashuka dimbani kuumana na wagosi wa kaya Coastal Union kutoka Jijini Tanga katika muendelezo wa kinyanganyiro cha kombe la ligi kuu Vodacom Tanzania bara.
Mtanange huo wa aina yake wanalamba lamba Azam FC watawakaribisha vijana kutoka Tanga coastal union katika uwanja wa Azam complex Chamazi, majira ya saa moja jioni kwa kiingilio cha shilingi 3000 kwa majukwaa ya mzunguko na 10000 kwa VIP.
Msimu huu michezo ya raundi ya kwanza Azam fc ametoka kifua mbele wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani ambapo mchezaji Obrey Chirwa aliifungia timu yake bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania,
Nao wagosi wa kaya Coastal Union hali ilikuwa mbaya kwa upande wao,ambapo walipoteza mchezo wake wa kwanza kwa matokeo ya 0-1 dhidi ya Namungofc katika uwanja wa Majaliwa Lindi.
Tujikumbushe katika michezo ya ligi kuu iliyoisha msimu 2019-20 Azam alionekana kuwa kibonde wa Coastal Union kwa kushindwa kufurukuta kupata alama 6 si nyumbani wala ugenini.
Mchezo wa raundi ya kwanza Azam akiwa ugenini katika dimba la uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga iliruhusu nyavu zake kutikiswa na Coastal Union kwa kufungwa bao 1-0 na kuondoka wakiwa hawajaambulia kitu.
Huku mchezo wa raundi pili pia Azam alipoteza tena alama 3 muhimu wakiwa katika uwanja wa nyumbani Azam complex kwa kutundikwa mabao 2 -1 na wagosi wa kaya.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...