SHIRIKA la ndege la kimataifa la Emirates limeendelea kukidhi mahitaji ya wateja kupitia huduma za anga, na hiyo ni kufuatia mrejesho kutoka kwa wateja kupitia safari za Dubai ambazo zimeonesha mafanikio ikiwa pamoja na kutoa fursa mbalimbali kwa wateja wao kupitia anga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Masoko wa shirika hilo Adnan Kazi imeeleza kuwa kwa sasa wateja wanaotumia usafiri wa anga, kupitia Emirates wanaweza kutembelea maeneo 30 zaidi na wateja kupitia ubia wa shirika hilo na 'FlyDubai' wanaweza kutembelea maeneo 70 zaidi, ikiwemo Zanzibar, Belgrade, Bucharest, Kyiv na Sofia.

Imeelezwa kuwa makubaliano Kati ya Emirates na FlyDubai yalianza mwaka 2017 na yakazaa matunda bora toka kwa wateja wao ambao wamekuwa wakifanikiwa na kufurahia safari zao za Dubai, na zaidi ya wateja milioni 5 walionesha mafanikio katika miaka miwili ya ubia huo.

Imeelezwa kuwa mahusiano hayo yataendelea  kuongezwa kwa nchi nyingi zaidi ili kujenga mtandao wa Kimataifa ambapo mpaka sasa FlyDubai tayari inafanya kazi katika vituo 32 tangu mwezi Juni na inatarajiwa kujitanua zaidi kwa miezi ya hivi karibuni.

"Emirates itaendelea kushirikiana na nchi katika Kuhakikisha huduma za usafiri wa abiria na mizigo inapatikana bila tatizo". Amesema Kazi.

Aidha taarifa hiyo imewataka, wateja watumie fursa hiyo kupitia Emirates na FlyDubai kupata mtandao wa miji kwa tiketi moja na kupata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali.

Kuhusiana na mlipuko wa virusi vya Corona (Covid-19.) Imeelezwa kuwa vipimo kwa wasafiri wote itakua lazima na hiyo ni pamoja na  kutoa huduma zote ikiwemo vitakasa mikono na barakoa na tayari wahudumu wote wamepata mafunzo ya namna bora ya kujikinga na virusi vya Corona.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...