Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, benki ya NBC Makao Makuu Bw Elibariki Masuke (katikati) akifafanua kuhusu huduma za benki hiyo kwa wadu wa sekta ya madini kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Bi Angellah Kairuki (wa pili kushoto) wakati Waziri huyo alipotembelea banda la benki hiyo lililopo kwenye maonesho hayo. Wengine ni pamoja na Waziri wa Madini Bw Dotto Biteko (wa tatu kushoto) pamoja na Meneja Mahusiano na Serikali wa benki hiyo Bw William Kallaghe (Kushoto)


 Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, benki ya NBC Makao Makuu Bw Elibariki Masuke (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Bi Angellah Kairuki baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza miongoni mwa  taasisi za kifedha na benki zilizoshiriki kwenye  maonesho ya Madini na Teknolijia yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani Geita. Wanaoshuhudia ni pamoja na Waziri wa Madini Bw Doto Biteko Kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.

 Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, benki ya NBC Makao Makuu Bw Elibariki Masuke akionesha moja ya tuzo ambazo benki hiyo ilifanikiwa kutwaa katika maonesho hayo.

 Muonekano wa tuzo hizo.

 Meneja Benki ya NBC Tawi la Geita Bi Hilda Bwimba akionesha  tuzo ambazo benki hiyo ilifanikiwa kutwaa katika maonesho hayo.

Wafanyakazi wa benki ya NBC wakishangilia na kujipongeza baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo hizo.



Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeibuka kinara kwenye Maonesho ya Madini na Teknolojia yaliyomalizika mwishoni mwa wiki  mkoani Geita ambapo taasisi hiyo imefanikiwa kutwaa jumla ya tuzo tatu ikiwemo tuzo ya mshindi wa kwanza kwa taasisi za kifedha na benki zilizoshiriki kwenye  maonesho hayo.

Benki hiyo pia ilifanikiwa kutwaa tuzo ya Mdhamini Mkuu wa maonesho hayo kwa taasisi za fedha huku pia ikifanikiwa kuibuka mshindi wa tatu wa jumla katika maonesho hayo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hizo na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji Bi Angellah Kairuki aliemuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkurugenzi wa Idara ya wateja binafsi, benki ya NBC Makao Makuu Bw Elibariki Masuke alisema tuzo hizo tatu zinaakisi mafanikio makubwa ambayo benki hiyo imeyapata  kupitia maonesho hayo.

“Kimsingi tuzo hizi tatu zinaakisi mafanikio makubwa ambayo benki ya NBC tumeweza kuyapata kupitia maonesho haya ikiwemo kuendesha program mbalimbali za mafunzo kwa wadau takribani 600 wa sekta ya madini wakiwemo wachimbaji wadogo na wajasiriamali.’’ Alisema

Aliongeza kuwa mkakati wa benki hiyo baada ya maonesho hayo ni kutekeleza kwa vitendo masuala muhimu iliyoahidi kuyafanya kwa kushirikiana na wadau hao ili kuboresha zaidi sekta hiyo.

Katika maonesho hayo benki hiyo pia  iliendesha huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti mpya kwa wateja, kuendesha kliniki ya biashara ambayo ilisaidia kukusanya maoni ya wadau wa sekta ya madini zaidi ya 150 ambao walikutanishwa na taasisi mbalimbali za serikali.

Aidha  kupitia makongamano mbalimbali benki hiyo iliwawawezesha wadau wa sekta ya madini kubadilishana mawazo baina yao wenyewe lakini pia baina yao na mamlaka mbalimbali za serikali ikiwemo Wizara ya Madini, TRA, NEMC, SIDO na TANTRADE, TABWA, OSHA,GST na NSSF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...