Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya James Kaji (kulia) akimtambulisha binti aliyekamatwa na Dawa za kulevya aina za Heroin Maria Mtambo (kushoto) alizosafirisha kupitia kifurushi cha vitabu, Kaji amewataka vijana kujiepusha na mahusiano hasi na raia wa nchi za Magaribi, jijini Dar es Salaam.

Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya James Kaji akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa juu ya ukamatwaji wa dawa za kulevya kwa mwezi Septemba ambapo ameonya wale wote wanaojihusisha na shughuli hiyo kuacha mara moja kabla ya kufikiwa na vyombo vya dola, leo jijini Dar es Salaam.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imefanikiwa kukamata takribani kilo 343.7 za dawa za kulevya aina ya Mirungi na Dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa gramu 448.14 katika matukio mawili tofauti kwa mwezi Septemba 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema kuwa katika tukio la kwanza, mnamo Septemba 17 mwaka huu Mamlaka hiyo ilimkamata Mary Edson Mtambo (25) kabila Mnyiha na mkazi wa Tegeta kwa Ndevu ambaye alikua akisafirisha kifurushi cha vitabu viwili ambavyo ndani yake kuliwekwa unga wa dawa za kulevya aina ya Heroin wenye uzito wa gramu 448.14.

Kaji amesema kuwa, binti huyo anajishughulisha na kazi za usafi huko Tegeta na aliyekuwa anamtumia kifurushi hicho cha dawa za kulevya ni mpenzi wake ambaye ni raia wa kigeni.

Aidha amesema kuwa katika nyakati tofauti mkoani kigoma iliwakamata watuhumiwa George Justine Mathew (21) kabila la Muha na mkazi wa Kigoma mjini akiwa na maboksi mawili yenye jumla ya  kilo 16.05 za majani makavu ya dawa za kulevya aina ya Mirungi katika eneo la kutuma na kupokea vifurushi, Posta Mkoani Kigoma.Aidha walimkamata Alex Benedict Ntiruka (31) kabila la Muha wa Kasulu Kigoma akiwa na maboksi mawili yenye jumla ya vifurushi nane vya majani makavu ya dawa za kulevya aina ya Mirungi yanayokadiliwa kuwa na uzito wa kilo 16, na alikuwa akifanya maandalizi ya kuyatuma katika eneo la Posta, Kigoma.

Jenerali Kaji amesema kuwa Mamlaka hiyo na Serikali wapo makini wakati wote na yeyote anayejihusiha na biashara hiyo atakamatwa na sheria itafuata mkondo wake.

Amesema kuwa wameendelea kufanya uchunguzi na kubaini mtandao wa usafirishaji wa dawa za kulevya aina ya Mirungi nje ya nchi na kufanikiwa kuwakamata washiriki wa mtandao huo na watafikishwa mahakamani.

 Pia amewashauri vijana kuwa makini na mahusiano na raia wa nchi za Magharibi ili waepukane na majanga hayo na amewashukuru wasafirishaji wa vifurushi wakiwemo Posta na DHL kwa ushirikiano katika vita ya dawa za kulevya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...