Na Samwel Mtuwa- Morogoro.
Timu ya wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa  Madini Tanzania (GST) wakiongozwa na Mtendaji Mkuu Dkt. Mussa Budeba wamefika katika wilaya ya Malinyi Kijiji Cha Misegese mkoani Morogoro kunasadikiwa uwepo wa Madini ya dhahabu.

 Wataalam hao  walifika katika eneo hilo kwa lengo la kukutana na wachimbaji wa eneo hilo , kufanya upimaji wa Miamba pamoja na kuchukua sampuli za miamba kutoka katika kila duara lililochimbwa kwa ajili ya Utafiti zaidi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa GST aliwashukuru wachimbaji hao wadogo kwa ushirikiano mzuri walionesha na kuhaidi kuwa sampuli zote zilizochukuliwa zitafanyiwa Utafiti wa jiosayansi na kuletewa mrejesho wa majibu.

Aidha kaimu Meneja wa mgodi huo Ismail Hanga aliwashukuru wataalam wa GST kwa kuweza kufika katika eneo hilo , akifafanua kuwa ujio wa wataalam umewapa motisha ya kuendelea na uchimbaji.
 
Eneo la uchimbaji lipo umbali wa kilomita 25 kutoka Malinyi Mjini, likiwa na wachimbaji wadogo takribani 50 lenye maduara 13 yanayoendelea kuchimbwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...