*Yawataka wakubali ukweli upepo wa uchaguzi mkuu mwaka huu hauko vizuri kwao

*Pia kimezungumzia kuimarika kwa diplomasia katika kipindi hiki cha Dk.Magufuli


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Chato

 CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Humphrey Polepole kimewatolea uvivu wagombea urais wa vyama vya upinzani ambao wamekosa uvumilivu na kushindwa kukubali kwamba upepo wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu hauko vizuri kwa upande wao na sasa wamebaki wakipotosha na kusema maneno ya uongo kwa umma.

Akizungumza leo Septemba 11,2020 wilayani Chato mkoani Geita wakati akitoa tathmini ya mwenendo wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli, Polepole amesema Chama chao safari hii kinafanya kampeni za kisayansi na ziko tofauti na miaka iliyopita na wamekuwa wakifuatilia wagombea wengine na kampeni zao.

"Hata hivyo baadhi yao wamekuwa wakitoa maneno ya kashfa, Chama cha bwana Freeman Mbowe(CHADEMA), kama kuna watu wamekosewa heshima na utu wao umekweza basi ni waandishi wa habari nchini, siku waliyokuwa wanazindua kampeni zao waliwaondoa TBC, wananchi wanafuatilia kwa njia ya live lakini unakwenda kufukuza watu.

"TBC walikuwa na kila kitu pale, wana magari, walikuwa wameshatandaza waya, wameweka kila kitu halafu unatoa dakika 15 wawe wameondoka.CCM inalaani kitendo hicho,maana kilichofanyika ni makosa, siku ile wanahabari wa TBC huenda wangepigwa, wangeuawa, na hao ndio viongozi ambao nao wanataka eti wachaguliwe,
mwingine amechomoka mapema sana leo, hayupo nchini, huyo bwana(hamkutaja) ameondoka anasindikizwa kama beberu,"amesema Polepole na kuongeza.

"Hata hivyo kumekuwa na upotoshaji mkubwa, sio desturi yetu, sio desturi ya sheria na kanuni za Uchaguzi Mkuu.Hivi  karibuni  wamesikika wakisema wamezuia kutumia helkopta, tunatamani wangetumia helkopta ili sisi tuchanje ardhini.Tumefuatilia na kujiridhisha ni uongo mtupu na tumefurahi Mamlaka ya anga imetoa ufafanuzi.

"Lakini unajiuliza nini dhamira ya kutoa maneno ya uongo, maana yake ni kutaka kutenegeza chuki kwa mamlaka hiyo ambayo iko chini ya Serikali ya CCM, hiyo ni hila, kwanza tumejiridhisha hawakuwa na ratiba ya safari siku ile.Pili usafiri wa anga unasimamiwa kwa sheria za kimataifa pamoja na sheria za viwango vya mamlaka ya anga Tanzania,"amesema.

 Pia anayeendesha ndege lazima awe amekidhi vigezo na kwamba rubani aliyetakiwa kuendesha helkopta hiyo umri wake hauko katika marubani  wanatakiwa kuendesha ndege."Watanzania wawangalie kwa makini wapinzani hao, maana ukiwafuatilia wana kila aina ya hila, tumegundua hilo na ukweli ni kwamba siasa za aina hiyo hazina mashiko, watanzania wanataka kusikiliza sera, mgombea wetu na CCM wanazungumzia tulikotoka , tuliko na tunakokwenda na nini ambayo tumepanga kufanya kwa maendeleo ya nchi yetu.

"Pia kuna upotoshaji kwa watumishi wa umma, unapotaka kuwazungumzia watumishi wa umma kuna vigezo kadhaa lazima uangalie, uchumi, utumishi na mambo ya kisheria.Tangu Dk.Magufuli ameingia madarakani hakuna mfumuko wa bei, hata kama mshara utakuwa mkubwa bei zikiongezeka utaisha mapema, lakini pia mfumo  mzuri wa kudhibiti uchumi na Tanzania inacheza kwenye tatu.


"Pia wale wenye mshahara wa shilingi 300,000 kwa mwezi kushuka chini hakuna kodi, hata hivyo kumekuwepo na ongozeko la watumishi kutotozwa kodi,tumeamua kufafanua jambo hili, ili kuwang’amua wapinzani ambao wamekuwa wakipotosha.Lakini mnafahamu kodi kwa watumishi wa umma ilikuwa digiti mbili na sasa imefikia dijiti moja, ukipunguziwa kodi ule mshahahara wako unaongezeka,"amesema Polepole.

Wakati huo huo amesema nidhamu ya matumizi ya fedha katika matumizi ya serikali yamekuwa makubwa mno, na ndio maana siku hizi kuanzia tarehe 20 ujumbe unaingia kueleza tayari Serikali ya CCM imefanya jambo."Maelekezo ya Rais Magufuli stahiki ya mtu aipate kwa wakati aipangie matumizi kwa wakati, mnyonge mnyongeni na haki yake mpeni".

 Pia amesema kuna viongozi wa upinzani ambao ni wa binafsi na wengine wamekuwa wakijifanya wao ndio wanajua kuliko wengine."Ni katika kipindi hiki cha Dk.Magufuli ambapo katika Bara la Afrika tumefanya mageuzi makubwa, ikiwemo ya kuingiza Kiswahili kuwa lugha ya rasmi kwa nchi za ukanda wa SADC, nafasi za walimu zimetangazwa Afrika Kusini, Namibia, na nchi nyingine nyingi tu.

 Kuhusu diplomasia, Polepole amesema wapinzani wamekuwa wakipotosha kwamba diplomasia ya Tanzania imeyumba lakini ukweli ni kwamba chini ya Dk.John Magufuli dipolamasia iko vizuri na imeimarika zaidi."Ameingia tu akwa Mwenyekiti Jumuiya ya Afrika Mashariki, akiwa huko ameacha alama, alisimamia nidhamu na matumizi ya fedha.

"Baadae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) na huko amekipigania Kiswahil, Tanzania kupewa hadhi ya kimataifa , amefanya kazi nzuri katika afya ameimarisha taasisi zikiwemo za umma kama MSD  ambayo ndio imepewa jukumu  la kununua dawa zote kwa ajili ya nchi za ukanda wa SADC.MSD imeibuka kinara na kidedea, na sasa dawa zote za SADC zinapelekwa na MSD,"amesema Polepole.

 Amesema ni Dk.Magufuli katika kipindi kifupi amefungua balozi nane."Ubalozi wa Catar uko vizuri na sasa mbuzi zinakwenda kila siku iendayo kwa Mungu, Sudai, Cuba tuna mahusiano makubwa, tunahusiano mkubwa na Islael, Uturuki nao tunashirikiana vizuri ndio maana hata reli yetu ya kisasa  inajengwa na Waturuki, Namibia kule ni mbali kweli ni nchi ambayo iko Kusini Magharabi mwa Bara la Afrika,wanatambua kazi yetu na katika kipindi cha miaka mitano wameomba uwepo ubalozi, Korea, Algeria kote huko tuko.Haya anakuja mwingine amefilisika na kuanza kupotosha tu.

"Mwingine anapita Mbagala amekaaa juu gari yake yuko peke yake anafika Ikwiriri anasema kuna diwani wa upinzani kapotea , unapozungumza kuhusu Ikwiriri, Kibiti na Mkuranga unaacha kovu katika maisha yetu, pale watu wa CCM wameumizwa, watendaji wa vijiji, jeshi la polisi wamekatishiwa maisha yao, halafu anapita mtu anaanza kutoa maneno ya uongo. Unapokuwa mgombea unawajibika katika mambo ya kitaifa tunasimama pamoja, siasa hizi  ambazo ni dhaifu sio nzuri,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...