Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Chato

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimetoa salamu za pole kwa familia na Watanzania wote kutokana na kifo cha aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kada wa Chama hicho Jaji mstaafu Mark Bomani aliyefariki dunia leo.

Akizungumza leo Septemba 11,2020, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Humphrey Polepole amesema kwa niaba ya CCM na kwa niaba ya Mgombea urais kwa tiketi ya Chama hicho Dk. John Magufuli, kwa masikitiko makubwa wanatoa pole kutokana na kifo cha Bomani.

“Kifo cha ndugu yetu Mark Bomani ambaye amehudumu katika Chama na Serikali kwa muda mrefu, amekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa kwanza Mtanzania, amekuwa kada mzuri sana wa CCM, amewahi kugombea Urais ila hakupata uteuzi lakini aliendelea kuwa mtiifu kwa Chama,

“Mungu amekuweke mahali pema, alikuwa Mdhamini wa Chama Cha Mapinduzi, tumepata msiba mkubwa sana , natoa pole kwa watanzania wote,”amesema Polepole kabla ya kuanza kuzungumzia tathmini ya mikoa ambayo mgombea wa CCM Dk.John Magufuli amepita kufanya mikutano ya kampeni ambapo amekutana na maelfu ya Watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...