Mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wameendelea na kazi ya kuunganisha kipande cha bomba la inchi 54 eneo la Bunju, lililosombwa na mafuriko kutoka Mto Mpiji.
Kukamilika kwa kazi hii kutaongeza kasi ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa maeneo ya Tegeta hadi Bagamoyo.
Matengenezo ya bomba hilo yanatarajiwa kukamilika jumapili lakini kusombwa kwa bomba hilo hakujaathiri usambazaji wa maji katika maeneo yanayohudumiwa na mtandao huo wa maji.
Mafundi wa DAWASA wakiendelea na kazi ya kuunganisha bomba la Inchi 54 lililosombwa na mafuriko kutoka Mto Mpiji.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...