Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

SHIRIKISHO La mpira wa kikapu Tanzania (TBF) limempongeza Henry Mwinuka kwa kuteuliwa na Shirikisho la mpira wa kikapu nchini Rwanda (FERWABA) kuwa Kocha Mkuu Msaidizi wa timu ya Taifa ya Rwanda.

Timu ya Rwanda inajiandaa kushiriki mashindano ya Afrika (Afrobasket) yanayotarajiwa kufanyika nchini Rwanda 2021. 

Kabla ya Ukocha, Mwinuka alikuwa mchezaji wa zamani wa timu kadhaa nchini zikiwemo Pazi, Savio na timu ya Taifa ya Kikapu ya Tanzania, 

Akitoa taarifa hiyo, Rais wa TBF Phares Magesa amesema Mwinuka licha ya kuwa mchezaji mahiri amewahi kufundisha timu kama UDSM Outsiders ya Tanzania, Patriots ya Rwanda na kufanikiwa kuchukua mfululizo ubingwa wa Rwanda na ubingwa wa kombe la FIBA Africa kanda ya tano na sasa wanashiriki Basketball Africa League (BAL).

Magesa amesema , hadi anateuliwa alikuwa ni Kocha Mkuu wa timu ya REG inayomilikiwa na Shirika la Umeme la Rwanda. 

Ameeleza, Katika msafara wa mwaka 2011 wa timu ya Taifa ya Tanzania kushiriki Mashindano ya FIBA kanda ya tano nchini Rwanda, Mwinuka alikuwa ni miongoni wa mwa wachezaji nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania na kwa kiasi kikubwa kuchangia safari yake ya mafanikio na baadae aliporejea nchini licha ya kuendelea kucheza na kufundisha alijiendeleza zaidi na akashiriki mafunzo kadhaa ya ualimu wa kikapu yaliyoandaliwa na TBF na kuendeshwa na FIBA.

Katika mafanikio yake, Mwinuka ni mmoja wa Makocha waliofanikisha kumuibua na kumsaidia sana Mchezaji nyota wa NBA Hasheem Thabeet. 

Kwa niaba ya Shirikisho na kwa niaba ya Watanzania wote wanampongeza sana Henry Mwinuka na kumtakia mafanikio makubwa zaidi katika majukumu yake hayo mapya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...