Meneja Uendeshaji wa Meridian Bet Carlo Njato akimkabidhi baadhi ya michango Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Jesca Kawegere.

Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Michezo ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet kwa kushirikiana na klabu ya Lions zimetoa misaaada mbalimbali kwa wagonjwa wa kansa kwenye hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Meneja Uendeshaji mkuu wa Meridian Bet, Carlo Njato alisema msaada huo ni moja ya kazi zao katika kurejesha kwa jamii.

Alisema hiyo ni mara nyingine tena kujitoa kwa jamii baada ya kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wa kituo cha mlima wa nipe matumaini, kilichopo Kinyerezi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam hivi karibuni.

"Dunia iko katika maadhimisho ya siku ya kansa, hivyo Meridian Bet kwa kushirikiana na klabu ya Lions tukaona na sisi tushiriki kuwafariji wagonjwa wa kanda katika hospitali ya Ocean Road," alisema.

Alisema wametoa misaada ya vifaa mbalimbali kwa wagonjwa wa hospitali hiyo ikiwamo dawa za meno, miswaki, sabuni, thermometer, mafuta ya vaseline, gloves, diapers za watu wazima na taulo za kike kwa wanawake.

"Kama kampuni tumeamua kurudishwa kwa jamii na kuungana na wenzetu wenye maradhi ya kansa katika kuwafariji na kuwapa msaada huo," alisema.

Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya kansa ya Ocean Road (ORCI), Jesca Kawegere aliwashukuru Meridian Bet na klabu ya Lions kwa upendo waliouonyesha kwa wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

"Wagonjwa wanaotibiwa hapa wengi wao wamekuwa na uhitaji mbalimbali wa kijamii, hivyo msaada huu ni faraja kubwa kwao, kama Taasisi tunawashukuru mno Meridian Bet na klabu ya Lions kwa upendo waliouonyesha kwa wagonjwa," alisema.

Gavana wa Lions Club Tanzania, Moiz Bakary alisema msaada huo ni moja ya wajibu wao kwa jamii.

"Klabu ya Lions kote nchini imewajibika kwa jamii kipindi hiki ambacho dunia iko kwenye maadhimisho ya siku ya kansa, hivyo kwa Dar es Salaam na Pwani wakishirikiana na Meridian Bet wametoa msaada huu, na mikoa mingine nchini klabu yetu imetoa misaada pia," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...