Mgombea Ubunge jimbo la Mkuranga, Abdallah Hamisi Ulega akizungumza na wanachama wa Chama cha Mapindunzi na Wananchi kijiji cha Kinene Kata ya Mwarusembe.
(Picha na Emmanuel Massaka michuzi Tv)

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Mkuranga kupitia  tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Abdalah Ulega amewataka wananchi wa kijiji cha Kikoo kilichopo Kata ya Kitomondo wilayani Mkuranga mkoani Pwani kuchagua CCM ili wapate maendeleo.

Ulega ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata hiyo ya Kitomondo katika mkutano wa kampeni katika vijiji viwili vya Kikoo pamoja na kiwambo.

Amesema vijiji hivyo vilikosa maendeleo miaka mitano iliyopita kwasababu vilikuwa na  kikiongozwa na diwani wa upinzani hivyo amewaomba wananchi  kuchagua CCM miaka mitano ili wapate maendeleo kwa kuchaguwa  Rais,Mbunge pamoja na diwani wa CCM

"Mkikichagua chama cha mapinduzi ccm kikoo itainuka,mtapata shule ,zahanati yenu ambayo ipo  kwenye gebo itamalizika   na nitatoa mifukoa mia ya Saruji muanze ujenzi wa nyumba ya mganga, ndugu nzangu   yalipota sindwele tugange yajayo " amesema Ulega
 
Aidha aliongeza kuwa anafahamu kwamba vijiji hivyo vinamatatizo mengi kutokana na diwani aliyepita hakuwa na ushirikiano na wananchi na kuwaomba wanavijiji hao, kuwa na umoja,ushirikiano na mshikamano kwa kuweka mafiga matatu ya Chama Cha Mapinduzi ili maendeleo yaweze kupatikana ikiwemo umeme ambao utafika vijiji vyote.

Akizungumzia barabaraba kuu ya Mwarusembe kuingia Kitomondo ambayo imeharibika kutokana na malori yanayopita kubeba udongo,Ulega amesema atafanya utaratibu wa kuzungumza na halmashauri ili magari hayo ya bebe mizigo kulingana na uwezo wa Barabara hiyo, atakama yanalipa kodi hili kuepusha huaribifu unaoendelea.

Ulega ambaye ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi aliendelea na kampeni katika kijiji cha Kinene kilichopo Kata ya Mwarusembe wilayani Mkuranga na kuwaahidi wananchi wa eneo hilo kuwapatia mradi mkubwa wa maji ili kuwaondolea changamoto kubwa ya maji wanayokumbana nayo.

Aidha amesema kupitia Ilani ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 yenye kipengele kinachounga mkono juhudi za vijana ,ameahidi kuwaunga mkono vijana wa kinene kuwapatia TV na Decoder ili waanzishe mradi wa kunyesha video utakao wakwamua kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuimalizia shule ya msingi ya kinene ili watoto waanze kusoma.

Amesisitiza miaka mitano iliyopita wamefanya kazi kubwa ya kusambaza umeme vijijini ikiwemo kijiji cha  kinene  na baada ya kushinda uchaguzi watahakikisha umeme unaenea katika vijiji vyote pamoja na  kuwatawatafutia kisima kikubwa cha maji.





Mke wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mkuranga koa wa Pwani ,Mariam Ulega (katikati) wakiwapamoja na wananchi wa kata ya Mwarusembe wakiburudika baada ya kukiombea kura Chama cha Mapinduzi.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Mkuranga mkoa wa Pwani,Abdallah Ulega akiwapokea wanachama mpya  kutoka chama cha upinzani katika kijiji cha Kiwambo kata ya Kitomondo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...