
MTK Helio G90T processor na RAM ya GB 8+ 128 ROM, vinaifaya Infinix ZERO 8 kuwa na ufanisi zaidi wa kufungua /kubeba videos na games zenye ukubwa wa aina yoyote pasipo kugoma goma. Vile vile Infinix ZERO 8 ina teknolojia ya 3D hii ni maalumu kwajili ya kupunguza joto endapo utaitumia simu yako kwa muda mrefu.
Infinix ZERO 8 ina kamera zenye kubeba megapixel kubwa, nyuma ikiwa ni 64 mbele 48 na IMX686 Sensor maalumu kwajili ya picha kali na zenye uhalisia pasipo kujali muda wala mazigira.
Infinix ZERO 8 inauwezo wa kudumu na chaji kwa zaidi ya siku moja kutokana na ujazo wake wa mAh 4500 na 33W Super change yenye battery kwa dakika chache.
Muonekano wa Infinix ZERO 8 ni wakitajiri, naweza sema ina design yenye kuvutia kutokana na umbo lake kuwa jembamba lenye kutawaliwa na wigo mpana wa kioo cha inch 6.85FHD+.
Kwa sasa Infinix ZERO 8 ipo Tanzania na unaweza kuipata katika maduka yote ya simu kwa bei isiyozidi Tsh.750,000/=





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...