Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Chato
RAIS wa Uganda Yoweri Museveni ameeleza hatua
kwa hatua kuhusu juhudi walizofanya kuhakikisha wanapata mafuta ambayo sasa
baada ya kukamilika kwa bomba la kuyasafirisha kutoka nchi kwake hadi Tanzania
yataanza kwenda kuuzwa kwenye soko la Dunia.
Ameyasema hayo leo Septemba 13,2020 wilayani
Chato mkoani Geita wakati akizungumzia ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta
ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga nchini Tanzania.
Ambapo ametumia nafasi hiyo kusisitiza kwamba
takwimu ambazo zimetolewa na Rais Dk.John Magufuli kuhusu yale ambayo
wamekubaliana ziko sawa.
"Sasa juu ya bomba, Rais Magufuli amelizungumzia
vizuri na takwimu zote wamezionesha, mapipa ya mafuta bilioni 6.5 ambayo ndio mafuta yanajulikana
kwa sasa na eneo ambalo limegundulika kuwa na mafuta ni asilimia 40 kati ya
eneo lote na ambalo limebakia tunaendelea kutafuta na matarajio yao ni kupata
mafuta mengi zaidi.
"Pia kuna sehemu nyingine imebainika kuwa
na mafuta.Bonde Albarti tunayo mafuta tayari kwani yanayonekana kwenye
kompyuta, lakini shida iliyoko kuna fujo kule , hatujapata muda wa kufuatilia.
"Wakati tunatafuta mafuta tulishirikiana na
Mabutu alipokuwa madarakani lakini ikashindana na baadae tukaona tufanye peke yetu.Tumetumia
watalaamu wetu mwanzo mpaka mwisho, watu wa nje walituchezea,"amesema Rais
Museveni wakati anafafanua jinsi walivyogundua mafuta.
Ameongeza kuwa Ulaya Mashariki baada ya kuanguka,
nchi ya Urusi nayo ilibaini inayo mafuta mengi sana ,hivyo kampuni nyingi za
kutafiti mafuta zikaelekeza nguvu katika nchi hiyo na wakaisahau Uganda.
"Wakawa wanasema wana wasiwasi mafuta
hayapo.Wakabadilika na kutuambia mafuta hayapo, tukahoji sasa mbona
wametugeuka, tukaamua kuagana nao.Hivyo tukapeleka watu wetu kwenda kusoma nje
na baada ya kurudi ndio wakafanya kazi hiyo na leo tunamafuta,"amesema.
Amesema mafuta yaligundulika mwaka 2006, hivyo sasa
ingekuwa imefika miaka 16 wanaendelea kuvutana na kampuni za mafuta na ingawa
wamechelewa lakini wamejifunza zaidi juu ya mafuta.
Kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda
hadi Tanzania, Rais Museveni amesema watu wake walikuwa wanagombania kodi
ambazo ndani ya miaka 25 zinakuwa dola milioni 800, lakini huo mradi uwekezaji
peke yake ni dola bilioni 16 kwa pande zote mbili,
"Hivyo nimeona hakuna sababu ya kuendelea
kuchelewesha mradi huu kwasababu ya kodi.Ni kama vile unapoanza shamba jipya na
ukaanza kulima kwa mara ya kwanza litakuwa na gharama lakini utakapolima tea
gharama zitapungua.
"Tuanze kupata hasara ya hapa na pale,
tukashaingia tutajifunza zaidi, tutapa fedha za kuendesha mambo mengine.Hawa
watu wangu ni wakali kwa Wazungu, niliwafundisha ukali na hiyo ni safi sana,"amesema
Rais Museveni.
Akifafanua zaidi Rais Museveni amesema
alizungumza na Rais Magufuli kwa simu kuhusu namna gani watagawana juu ya mrad."Kwasababu
kama ambavyo mmesikia sehemu kubwa mradi uko Tanzania.
"Kwa hiyo nielezea kama unataka kuchukua asilimia
70 kwa asilimia 100 we chukua tu, kama ni asilimia 80 kwa asilimia 100 ni nyingi
sana. Tumekubaliana 60 inakuja Tanzania na 40 inakwenda Uganda, kwa hiyo
nafurahi.Kama mnavyosikia hivi karibuni tutakuja kuzungumzia gesi, Uganda
tunamahitaji ya gesi.
"Uganda inaonekana kuwa na mafuta, gesi ipo
lakini ni kidogo, tunataka gasi kwa ajili ya vyuma vya pua na mambo mengine,
kwa hiyo nashukuru ile ofa yako Rais Magufuli kwamba pale bomba la mafuta
litapita basi bomba la gesi litapita, sasa huo ndio undugu,amesema Rais
Museveni.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe.
Yoweri Kaguta Museveni akiongea baada ya kutia saini Waraka wa Pamoja
Unaoagiza kuanza haraka mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima
(Uganda) hadi Tanga (Tanzania) kwenye sherehe fupi iliyofanyika Uwanja
wa Ndege wa Chato mkoani Geita leo Jumapili Septemba 13, 2020



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...