Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

MCHEZAJI Wa timu ya wanawake ya Mpira wa Kikapu JKT Jesica Ngisaise ameingia katika historia ya wachezaji waliofunga pointi nyingi zaidi ya 100 duniani. 

Jesica alifunga pointi 105 peke yake katika mchezo (JKT Vs Ukonga Princess) katika Ligi ya Kikapu ya wanawake (RBA) inayoendelea jijini Dar es Salaam. 

Jesica pia ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania na ameshiriki matukio na Michezo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Senegal, Kenya na Afrika Kusini ambako alishiriki kambi Basketball Without Border 2018.

Katika kambi hiyo, Jessica alifanikiwa kuchaguliwa katika timu ya nyota bora wa Afrika ya Wasichana na kucheza mchezo wa utangulizi kabla ya mchezo wa NBA uliofanyika Sun Arena, Pretoria, 2018. 

Kupitia kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini TBF Phares Magesa, Shirikisho limempongeza Mchezaji huyo kwa kuweza kuingia katika historia kubwa kwake ya kufunga pointi 105 kwenye mchezo mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...