Na Said Mwishehe,Michuzi TV -Mwanza
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dk.John Magufuli amewaahidi wananchi wa Mkoa wa Mwanza iwapo watamchagua tena kuwa Rais kwa miaka mingine mitano atahakikisha anaendelea kuifanya Mwanza kuwa kituo cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki.
Dk.Magufuli amesema hayo leo Septemba 7, 2020 mbele ya maelfu ya wananchi wa Mwanza ambao walifika kusikiliza alipokuwa kwenye mkutano wake wa kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28,2020.
Wakati anafafanua miradi ya maendeleo ambayo imefanyika katika Mkoa wa Mwanza alitumia nafasi hiyo kukumbusha ahadi ya kuifanya Mwanza kuwa kituo cha kibiashara na mkakati wa kwanza ulikuwa ni kufanya mambo mawili ambayo ni ujenzi wa miundombinu na kuboresha, na kuimarisha huduma za kijamii.
Amefafanua kazi ambayo itakwenda kufanyika iwapo wananchi hao watampa ridhaa ya yeye na Chama chake kushinda uchaguzi mkuu, hivyo basi Serikali itahakikisha Mwanza inakuwa kituo cha biashara na ili kufanikisha hilo ndio maana Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 imefafanua kwa kina yale ambayo yanakwenda kufanyika ili kufanikisha mkakati huo.
Ameeleza jinsi ambavyo Serikali katika kipindi cha miaka mitano ilivyoweka nguvu katika kuimarisha usafiri wa barabara, uwanja wa ndege na meli kwa ajili ya kusafirsha wananchi wanaozunguka Ziwa Victori ikiwa pamoja na mkakati wa kununua meli mpya moja na kufanya ukarabati wa meli tano katika ziwa hilo.
"Iwapo mtatuchagua katika uchaguzi mkuu mwaka huu tutahakikisha meli zinatoka hapa Mwanza na kwenda katika nchi za Uganda na Kenya pamoja na maeneo mengine ya mikoa inayozunguka Ziwa Victoria.
"Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumefungua milango ya kibiashara kati yetu na nchi jirani na huo ndio mpango wetu , ndio maana tumekuja tena hapa kuwaomba kura tukakamilishe yale ambayo tumeanza kuyafanya."amesema Dk.Magufuli.
Katika mkakati huo wa kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa kituo cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki, Dk.Magufuli amesema Serikali imekuwa na mkakati wa kupanua uwanja wa ndege wa Mwanza na kazi hiyo ilishaanza , hivyo ndege zitakuwa zikianzia Mwanza kwenda nchi za Ulaya moja kwa moja, hivyo kufungua fursa za kibiashara na uchumi kwa Mwanza.
"Katika kipindi cha miaka mitano tumenunua ndege 11 na mkakati wetu iwapo tutachaguliwa tutanunua ndege nyingine mpya tano, katika hizo moja itakuwa ndege ya mizigo ambayo nayo itasaidia kwa wale wanaosafirisha mizigo yao kwa kutumia usafiri wa anga,"amesema Dk.Magufuli na kusisitiza wanaoweza kufanya hayo yote kwa Mwanza ni CCM
Amezungumzia pia ujenzi wa reli ya treni ya kisasa ya kutumia umeme ambayo ujenzi wake ulishaanza kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na tayari wameshatangaza kuanza ujenzi kuanzia Dodoma Iasaha kuja Mwanza, hivyo Mwanza inakwenda kuendelea kufunga katika usafiri wa reli na hivyo usafiri huo utatumika kwa watu kufanya shughuli zao za kila siku kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.
Dk.Magufuli wakati anaelezea mkakati huo alikumbusha Mwanza ilivyokuwa huko nyuma ambapo hata barabara nyingi zilikuwa mbovu na kusababisha hata kwa wale wanaosafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam kwa kupitia nchini Kenya na wale Kagera kupitia Uganda.
"Kwa nguvu zote ambazo tumefanya katika masuala mbalimbali, Mwanza ni mashahidi huko nyuma ukitaka kusafiri lazima upite nchi jirani, ukitoka Mwanza lazima uende mpaka Kenya, kisha arusha Dar es Salaam.
"Hata Kagera ilikuwa lazima upite Uganda, ilikuwa nchi ya ajabu unakwenda kwenye makao makuu ya nchi yao, unapita kwenye nchi nyingine,"amesema Dk.Magufuli huku akitumia nafasi hiyo kuelezea mikakati mbalimbali ya maendeleo inayokwenda kufanyika Mwanza ."Tumekuja kuomba kura ili tukafanye kazi ambayo tumeinza."
Amewakumbusha kwamba anaeleza hayo na kufafanua mipango ya Serikali ili ikifika Oktoba 28 wananchi wawe na uamuzi sahihi huku akisisitiza Mwanza imebadilika sana."Kila ukienda unakuta nyumba nzuri zinaendelea kujengwa.
"Mipango ya baadae hakuna mtu kubolewa nyumba yake huko juu milimani, Serikali yenye mpango mizuri itapeleka huduma zake huko huko, kaaeni kwa raha na ndio maana naomba mniachie hawa wabunge wa Mwanza kwasababu watakwenda kutekeleza Ilani ya uchaguzi mkuu".

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano
wake wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumatatu Septemba 7, 2020

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...