MGOMBEA Wa kiti cha Ubunge katika Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali amezindua rasmi kampeni katika jimbo hilo, uzinduzi uliofanyika katika Kata ya Ziba.

Katika uzinduzi huo Gulamali amewashukuru wananchi wa Manonga kwa ushirikiano uliotukuka walioonesha kwa kipindi cha miaka mitano na kuahidi neema na kuleta maendeleo zaidi katika sekta za Elimu, Afya na Miundombinu.

Pia amewataka wananchi wa Manonga na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi siku ya Oktoba, 28 mwaka huu kupiga kura kwa Rais. Dkt. John Joseph Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM ili kuendelea kuleta maendeleo zaidi.

Katika uzinduzi huo Gulamali aliambatana na mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...