Na Khadija seif, Michuzi tv
MWANAMZIKI kutoka nchini Nigeria ambae pia ni mkali wa kibao kinachokwenda kwa jina la Baby, Joe Boy Wurld wa Surz pamoja Singah alieimba Teamo wanatarajiwa kutua bongo mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kampuni ya str8up vibes, Sniper Montana amesema ameamua kuikata kiu ya Mashabiki wote wanaopenda muziki.
"Kutokana na kuzuka kwa janga la ugonjwa wa Covid 19 tulisitisha shughuli zote za kutoa burudani kwa Mashabiki wetu na kupelekea mipango mingi kuvunjika hivyo tumerudi Tena kwa kishindo kikubwa na septemba 26 mwaka huu tunatarajia kufanya show."
Hata hivyo Montana amewaambia wasanii wakibongo iwe fursa kwao nakuchukua ujuzi kutoka kwa wanamuziki hao kutoka Nigeria.
Pia Mkurugenzi wa Operesheni katika kampuni hiyo, Andrew Mpepo amesema wapenda mziki mzuri pamoja na wadau waendelee kupitia kurasa wa mitandao ya kijamii wa kampuni ya str8up vibes.
"kuhusu kiingilio na wapi show hiyo itafanyika,wasanii wa nyumbani watakaopata nafasi kutumbuiza pamoja na wasanii kuwasili kwa wakali hao kutoka nchini Nigeria."
Kwa upande wake Lilian Kanora ambaye ni Meneja bidhaa wa Benji ya CRDB na moja ya wadhamini wa show hiyo, amesema wao katika shughuli hiyo watahusika katika kununua tiketi na pia kufanya matumizi kwa kuitumia kadi zao za 'tembocard'.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...