Na Lusajo Frank, Michuzi Tv
KIMBUNGA Sally kimepiga mwambao wa karibu na mpaka baina ya majimbo ya Alabama na Florida Kusini mwa Marekani, kikiambatana na mafuriko na upepo unaokwenda kwa kasi ya km 165 kwa saa.

Mamia ya watu wamelazimika kuokolewa baada ya nyumba zao kujaa maji.
Kimbunga hicho kimesomba boti yaliyokuwa ufukweni na kuyatupa nchi kavu, na kuangusha miti na kuezua nyumba katika miji ya Pensacola na Mobile.

Nyumba zipatazo 540,000 za makaazi ya watu na biashara zimeachwa bila umeme katika eneo hilo la kaunti ya Escambia, ambako maafisa wamesema watu 377 wameokolewa kutoka nyumba zilizofurika maji, ikiwemo familia ya watu wanne ambao walikuwa wamepanda mitini kuepuka kumezwa na mafuriko.

Hali ya hatari imetangazwa katika baadhi ya miji ya mwambao katika jimbo la Alabama, wakati vikosi vya kitaifa vya uokozi vikisubiriwa kuwasili katika majimbo yaliyoathiriwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...