MWENYEKITI Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM,) na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) Komred Kheri James (MCC) amezindua kampeni za Ubunge jimbo la Kawe hii leo kwa kumnadi Mgombea wa Ubunge kupitia CCM Askofu Josephat Gwajima pamoja na mambo mengine amewahimiza wananchi juu ya umuhimu wa kukichagua Chama cha Mapinduzi na wagombea wake wa ngazi zote.
Pia amesisitiza Wanasiasa kufanya kampeni za kistaarabu na amani.
Uzinduzi huo umefanyika Bunju na kuhudhuriwa na Viongozi, Wanachama na Wananchi wa wilaya ya Kinondoni wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Kate Kamba na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Kinondoni.











Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...