Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
TIMU ya Mtibwa Sugar imepoteza mchezo wake wa Kwanza wa Ligi baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa mabingwa wa kihistoria Yanga.

Mchezo huo uliochezwa leo ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro majira ya saa 10 jioni uliweza kukata mzizi wa fitna kwa Yanga kuibuka na ushindi huo.

Hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza hakuna timu iliyoona lango la mwenzie huku timu zote zikishambuliana kwa zamu kusaka goli la kuongoza.

Beki Lamine Moro akiwa nyota wa mchezo huo, aliweza kuisaidia timu yake kupata alama tatu kutoka kwa wakata miwa wa Turiani akimalizia kona safi iliyopigwa na Carlinhos dakika ya 61.

Mechi hiyo iliyokua na ushindani mkubwa, ilishuhudia dakika 90 za mchezo zikimalizika kwa Yanga kupata alama tatu kibindoni na kufikisha alama 10 sawa na mahasimu wao Simba.

Unakuwa ni mchezo wa pili Lamine kuipatia Yanga alama tatu baada ya ule wa Mbeya City katika Uwanja wa Mkapa nao akimalizia kona ya Carlinhos.

Sasa Yanga inarejea jijini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Coastal Union baada ya kumaliza michezo miwili nje ya Dar es Salaam dhidi ya Kagera na Mtibwa Sugar.

Baada ya matokeo hayo Azam wanaendelea kushikilia msimamo wa Ligi wakiwa na alama 12 wakishindwa michezo yote mitatu huku Simba na Yanga wote wakiwa na alama 10.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...