Taasisi ya kifedha ya FAIDIKA imezindua utaratibu wa kununua mikopo ya wakopaji kwenye mabenki na taasisi nyingine na pia kutoa mikopo mipya yenye riba nafuu baada ya kununua mikopo hiyo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Faidika, Baraka Munisi alisema kuwa huduma hiyo inatolewa kwa wafanyakazi wote wa serikali wenye mikopo katika mabenki na makampuni mengine.

Munisi alisema kuwa lengo la kuanzisha mpango huo ni kusaidia wakopaji ambao kwa sasa wanalipa riba kubwa na kuwa na marejesho makubwa yanayokatwa katika mishahara yao na kufanya kushindwa kufikia malengo ya maendeleo waliojipangia wakati wa kuchukua mkopo yao ya awali.
Alisema kuwa sababu nyingine ni kuwawezesha wakopaji kupata mwamko mpya wa kufikia malengo yao ambayo yalionekana kutofikiwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo kutoweza kupata mikopo mikubwa yenye marejesho ya muda mrefu.

“Tumeamua kutoa fursa kwa kila Mfanyakazi wa Serikali kupata mkopo mpya wenye riba nafuu na kulipiwa mkopo wake wa sasa wenye riba kubwa,  FAIDIKA ni moja ya microfinance inayotoza riba ndogo na kutoa mikopo yenye muda mrefu wa marejesho kuliko microfinance nyingine nchini,” alisema Munisi.

Alifafanua kuwa ununuzi wa mikopo ya mabenki na taasisi nyingine utafanyika kwa haraka bila kumchelewesha mkopaji (mteja) ambapo FAIDIKA itanunua na kuwapa mikopo ya kuanzia Sh 200,000 mpaka Sh millioni 70.

Alisema kuwa muda wa mrejesho ya mkopo utakuwa kuanzia miezi sita (6) mpaka miezi 84 kulingana na matakwa ya mteja; Mahitaji makubwa ambayo mkopaji anatakiwa kuwa nayo ni pamoja na taarifa ya deni kutoka kwa kampuni au benki uliyokopa iliyoidhinishwa na kugongwa muhuri.
“Pia mkopaji anatakiwa kuwa na kitambulisho cha kazi kikiambatanishwa na kitambulisho cha taifa au pasipoti au kitambulisho cha mpiga kura au leseni ya udereva pamoja na picha moja ya pasipoti,” alisema.

Kwa mujibu wa Munisi, pia mkopaji anatakiwa kuwa na stakabadhi moja ya mshahara wa mwezi uliotangulia na taarifa za kibenki kuanzia miezi miwili na kuendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...