*Sasa waahidiwa kujengewa uwanja wa ndege iwapo wataichagua tena CCM kushika dola


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Simiyu

SERIKALI ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk.John Magufuli umepeleka mabilioni ya fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ikwemo inayohusu barabara, maji, nishati, afya, elimu, kilimo , ufugaji na uvuvi.

Wakati Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk.John Magufuli akizungumza na maelfu ya wananchi wa mkoa huo wa Simiyu ameeleza kwa kina mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Akizungumzia miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Simiyu amesema kuna mabadiliko makubwa sana yamefanyika mkoani Simiyu licha ya kwamba mkoa huo ni mpya lakini maendeleo yake kama yana miaka 50.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo ya maendeleo ni ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo imegharimu Sh.bilioni 206.2 kwa ajili ya barabara za lami na barabara za changarawe , mradi wa Hospitali ya rufaa mkoa, ujenzi wa hospitali tatu za Bariadi, Busega na Itilima, ujenzi wa vituo vya afya vitatu na zahanati 14 pamoja na kupelea dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.bilioni 15.86 na kwamba fedha yote katika sekta ya afya ni Sh.bilioni 32.3.Huduma za afya zimeonggezeka, wanaojifungua kwenye vituo vya afya wameongezeka hadi kufikia asilimia 88, vifo vya watoto vimepungua, walikuwa wanakufa 362 sasa wanakufa watoto100.

Dk.Magufuli amesema Sh.73.8 zimetumika katika elimu ikiwemo kutengeneza madawati, kujenga nyumba za walimu, mabweni, kukarabati shule kongwe za Bariadi, wameajiri walimu wapya , kupeleka vitabu kwa shule za msingi na sekondari.

“Bariadi Mjini kilometa saba zimejengwa kwa lami huku nishati Sh.bilioni 81.1 zimetumika na vijiji 299 vimepata umeme, na sasa tunaendelea na mradi wa kituo cha kupooza umeme wenye kugharimu bilioni 75 kule Imalilo, ukishafika Imalilo ndio unasambazwa maeneo mengine yote, kabla ya kwenda kwingine lazima ufike hapo upozwe.Eti haya yote ni madogo, hayafai, halafu mtu apite aseme haya yote ni ya hovyo,”amesema Dk.Magufuli.

Kuhusu kilimo na ufugaji Dk.Magufuli amesema wananchi hao wa Simiyu wanafahamu kwamba anawapenda wafugaji na wakulima. ”Sitaki wafugaji wawe wanahamishwa, tunataka wakulima na wafugaji waishi pamoja.Mmeona hata kwenye samaki wameongezeka, kwenye mifugo nako wameongezeka.

”Simiyu mnalima sana pamba na nusu ya pamba inayopatikana inalimwa Simiyu, kulikuwa na changamoto ya kuchelewa kwa malipo lakini kutokana na changamoto ya Corona pamba haikuweza kupelekwa kule inakouzwa.Ulaya ndio soko letu la pamba lilipo lakini hawakwepo watu wa kuja kununua kwasababu watu walikuwa wamejifungia ndani ya nyumba(Lockdown).

”Ndio maana Serikali imetoa Sh.bilioni mbili kwa ajili ya kulipa madeni na tunataka badala ya kusafirisha pamba nje tunataka tutengeneze hapa hapa kama ni kutengeneza kanga au kitu chochote viwe vinatengenezwa nchini kwetu, hiyo ndio mipango tuliyonayo, ndio maana tunasimama hapa kuomba kura,”amesema Dk.Magufuli akielezea fedha ambazo zimetumika katika mkoa huo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wa viwanda amesema katika Mkoa wa Simiyu kuna viwanda 1,154 vidogo na vya kati kikiwemo kiwanda cha chaki huku akifafanua yake ambayo yamepangwa kufanyika katika mkoa huo iwapo watapata ridhaa Watanzania kuongoza tena kwa miaka mitano mingine vimeelezwa katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu yenye kurasa 303.

”Ilanii ina kurasa 303 na yanayohusu Simiyu yako ukurasa wa 21, 54, 57, pia yamezungumzwa ukusara 64, 65, kwa mfano , uk 66 barabara , uk 67 barabara.Ninayosema hayatoki kichwani yapo kwenye Ilani, uongozi hauhajaribiwi kama limao, uongozi unapimwa, na sisi mmeshatupima vya kutosha,

“Yamezungumzwa mengi kila ukurasa yamezungumzwa .Ukurasa wa 75 unazungumzia barabara pia na mengine mengi ndugu zangu.Haya tumeyapa na kuweka kwenye Ilani tunataka kujenga nchi, bila miundombinu bado , bila mipango hujatengeneza.Simiyu tutatengeneza kiwanja cha ndege,

”Siku nyingine ndege itatua hapo badala ya kwenda Mwanza ,na hivyo mtu atakuwa na uamuzi wa kuamua kusafiri kwa ndege au kwa barabara na mambo yanayohusu ndege yapo ukurasa wa 90.Mawasiliano yamezungumzwa katika ukusara wa 95, kusimamia mageuzi makubwa sekta ya madini yapo ukurasa wa 105, Simiyu imezungumzwa, katika mambo ya utalii katika Ilani hiyo,”amesema.

Pamoja na mafanikio lukuki ambayo yamefanyika Simiyu, Dk.Magufuli amesema anafahamu bado zipo baadhi ya changamoto ikiwemo ya wananchi kutaka umeme wa REA.Bariadi naomba mtuamini,tumetoka mbali, tuko mbali na tunakwenda mbali, kikubwa tumtangulize Mungu ikifika Oktoba 28 wakapate kura .Ninaomba hiyo tarehe 28 mkawapigie kura madiwan wote, wabunge wote,”amesema Dk.Magufuli.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bariadi katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa Bariadi mkoani Simiyu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...