Na Woinde Shizza, Michuzi TV Arusha
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Karatu kupitia Chama Cha mapinduzi Daniel Awack
amewahidi wananchi wa Jimbo hilo waliopo katika kata ya Mang'ola
kuwajengea shule ya bweni ya wasichana Ili kupunguza tatizo la mimba
kwa wasichana wa Jimbo Hilo
Aliyasema
hayo Jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo hilo ulioufanyika
katika kiwanja cha Mang'ola barazani uliopo katika kata hiyo, ambapo
alifafanua kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakishindwa kuendelea na masomo
kutokana na kupata mimba kipindi wakiwa shuleni
"Kumekuwa
na tatizo la mabinti wetu kupata mimba wakiwa shuleni na hii inatokana
na vishawishi wanavyovipata huko njiani wakati wakielekea shuleni, sasa
nawaahaidi mkinipa Kura zenu nitahakikisha najenga shule ya wasichana ya
bweni ambayo itasaidia kupunguza tatizo hili kwani wanafunzi watakuwa
wanakaa shuleni namaanisha katika mabweni hivyo itasaidia kuepuka
vishawishi ambavyo wanapata wakiwa njiani "alibainisha Awack
Aidha
pia aliwahidi wananchi wa Jimbo Hilo kuwawekea wakili ambaye atakuwa
anawasaidia katika kesi zao ili wasiweze kuzudhulumiwa katika kesi zao
mbalimbali,ambapo pia alibainisha katika Jimbo la Karatu kumekuwa na
changamoto ya barabara kwa kipindi Cha muda mrefu na kuwaahidi kuwa iwapo
watampa nafasi ya kuwawakilisha bungeni atahakikisha barabara hiyo
inajengwa katika kiwango Cha lami
"Najua
hapa Mang'ola wananchi wengi wanategemea kilimo Cha umwagiliaji na
tatizo lao kubwa Ni uhaba wa visima pamoja na miundo mbinu ya
umwagiliaji,nadhani mnanijua Mimi mwenyewe ni mkulima mkininipa kura
matatizo yote haya nawahidi nitayamaliza "alifafanua Awack
Akiongea
wakati wa kumnadi mgombea ubunge huyo pamoja na kumuombea Rais Kura
mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe alisema kuwa
wamchague Dr magufuli kwakuwa Ni miadilifu ,mtetezi wa
wanyonge,mchapakazi, mwanamapinduzi wa kweli,Ni kiongozi mpenda
haki,anachukia rushwa ,anachukia ufisadi na pia ni mtetezi wa yale
anayoyaamini hivyo wasiache kumchagua na katika kipindi chake Cha miaka
mitano ametekeleza ahadi zake zote kwa vitendo.
Naye
mgombea udiwani wa kata ya Qurus Danstan Panga aliwataka wananchi wa
Karatu kumchagua mbunge huyo kwa kuwa Kwanza Ni mkazi wa Jimbo lao pia
ni mtoto wa mkulima hivyo ataweza kupeleka matatizo yao bungeni ili
yaweze kutatuliwa .
"ndugu
Wana Karatu tumeongozwa na upinzami miaka 25 hapa lakini hakuna
Maendeleo yoyote tulioletewa barabara Ni mbovu ,huduma za afya atupati
vyema ,shule za bweni kwa watoto wetu wakike niseme tu 25 imetosha
tunaitaji mabadiliko ninaomba tusifanye makosa ya nyuma"alisema Panga
Akimuombea
Kura mgombea Urais kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi ambaye pia Ni
mwenyekiti wa CCM taifa pamoja na mgombea Ubunge Jimbo la Karatu
,Balozi Batilda Burian aliwataka wananchi kuwapa Kura za kishindo
wagombea hawa ili wakaweze kuwaletea Maendeleo na kuwasisitiza wafuate
kauli mbio yao inayosema miaka 25 ya kuongozwa na ushindani inatosha
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Steven Zelothe akimkabidhi mgombea Ubunge Jimbo la Karatu Daniel Awack ( kulia) ilani mbili za Chama cha mapinduzi katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Jimbo Hilo
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Karatu Daniel Awack akiomba Kura kwa wananchi wa Jimbo Hilo katika uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mang'ola barazani Jana

Baadhi ya Wafuasi na wanachama wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
Wabunge wa viti maalumu mkoa wa Arusha pamoja na mgombea Ubunge Jimbo la Longido wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Karatu
Bbalozi Batilda Burian akiwa amepiga magoti kwa wananchi wa Jimbo la Karatu kumuombea Kura mgombea Urais pamoja na mbunge wa Jimbo la Karatu Daniel Awack.
Aliekuwa mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Joshua Nassari akimuombea Kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Karatu ambapo aliwaambia wanakaratu waachane na vyama vinavyopenda fujo badala yake wahamie na wachague viongozi watakaowaletea Maendeleo (picha zote na Woinde Shizza ,Michuzi TV Arusha)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...