Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mara

WAGOMBEA ubunge katika majimbo mbalimbali yaliyopo mkoani Mara kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) wamewaomba wana Mara kuhakikisha katika uchaguzi mkuu mwaka huu wanamchagua mgombea urais Dk.John Magufuli ili apate miaka mitano mingine.

Wamesema kipindi cha miaka mitano ya utawala wa Rais Magufuli, kuna maendeleo makubwa yamefanyika mkoani hapa kwa kupelekewa maendeleo ya kila aina na hivyo wananchi wa mkoa huo wananchi wamchague ili endelee kuwaletea maendeleo

Wakizungumza mbele ya maelfu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa CCM Dk.Magufuli wabunge hao kwa nyakati tofauti wameeleza mambo ambayo yamefanyika katika majimbo ya mkoa huo.

Mgombea ubunge wa jimbo la Butiama Jumanne Sagini ambaye amepita bila kupingwa na kata zote 14 madiwani wamepita bila kupingwa amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kura zote ni kwa Dk.Maguguli na hiyo inatokana na maendeleo yaliyofanyika katika jimbo hilo na mkoa kwa ujumla.

”Nimesimama kumuombea kura Rais wangu, ambaye kwa sasa ndio mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa Oktoba 28 mwaka huu.Iko hospitali ya wilaya imewekwa vitendea kazi, vyumba vya upasuaji , vifaa vya kujifunguli akina mama, vituo vya afya viwili,

“Tunajua zipo kata ambazo vituo vya afya havijajengwa lakini wananchi wameanza kwa kujenga maboma na kazi iliyobakia ni kukamilisha. Tumpe mgombea urais wetu ili apate nafas ya kwenda kumaliza kazi aliyoanza katika mitano iliyopita yenye mafanikio makubwa,”amesema.

Amesema Dk.Magufuli katika utawala wake amefanikisha kuondoa changamoto ambazo zilikuwa zinawakabili wajasiriamali wadogo pamoja na wananchi wanyonge lakini hivi sasa watu wanaendelea na shughuli zao bila usumbufu.

Kwa upande wa mgombea ubunge Jimbo la Mwibara Charles Kajege amesema watu wote wana macho, wana masikio, “hivyo ni mashuhuda wa kazi nzuri zinazofanywa na Raisa magufuli.”Rais Magufuli ana sifa zote na wana Mwibara tayari tumeshaamua kura zote zinakwenda kwake.

Mgombea ubunge jimbo la Rorya Jafari Chege amesema kazi kubwa iliyopo mbele yao ni kumuombea nyingi Dk.Magufuli huku akitoa sababu zinazosababisha apewe tena miaka mitano kuongoza nchi yetu.

Amesema katika jimbo la Rorya kabla ya Rais Magufuli walikuwa wanapata fedha za maendeleo Sh.bilioni 13 lakini sasa hivi wanapata fedha Sh.bilioni 28 kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

“Kutokana na fedha hizo tunayo Hospitali ya Wilaya, aliahidi vituo vya afya na sasaa tunavyo viwili, tumejenga shule za msingi na sekondari nyingine kupitia fedha hizo.Tumepewa fedha sh.bilioni saba kwa ajili ya maji,”amesema na kutumia nafasi hiyo kuwoamba wananchi wa mkoa huo kumchagua Dk.Magufuli ili aendelee kufanya kazi ya kuleta maendeleo.

Amefafanua Rais Magufuli amewaamini vijana wengi kwa kuwapa nafasi katika utumishi wa umma na taasi nyingine zilizokuwa chini ya Serikali, hivyo ni jukumu la vijana kuhakikisha mgombea huyo wa urais anarudi tena madarakani kwa miaka mingine mitano


Wakati huo huo mgombea ubunge jimbo la Bunda Boniface Mwita Getere amesema kwamba kazi ya kumuombea Rais kura ni nyepesi sana kwani mwenyewe alishaifanya kwa miaka mitano kutokana na kazi aliyokwisha ifanya ya kuleta maendeleo.

”Mkoa wa Mara umepata maendeleo makubwa sana, tumepata hospitali ya mkoa, tumepata uwanja wa ndege, tumapata maendeleo kila eneo na hivyo ni jukumu letu mkoa wa Mara kumpa kura nyingi Dk.Magufuli,”amesema.

Amesema kwenye jimbo lake Rais Magufuli amempa hosptali ya wilaya, vituo vya afya viwili, vijiji vitano 35 vimepata umeme pamoa vitongoji 35 navyo vina umeme,wamepata barabara , hivyo hakuna sababu ya kumnyima kura.

Mgombea ubunge viti maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa amesema Oktoba 28 mwaka huu wananchi wa mkoa huo wana jambo lao na jambo lenyewe ni kumchagua Dk.Magufuli ili aongeze nchi yetu kwa miaka mitano. ”Rais Magufuli katika utawala wake ameboresha maisha ya wananchi wote wa Mkoa wa Mara, hivi sasa wako huru kufanya shughuli zao, chini ya utawala wake hata sisi wauza mboga za majani tunaweza kupata nafasi ya kugombea ubunge wakati huko nyuma ilikuwa ngumu,”amesema.

Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akinadi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 ambayo ikiwa na ukurasa zaidi ya mia tatu ni kubwa mara tatu zaidi ya ile ya mwaka 2015
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...