Na Amiri
Kilagalila,Njombe
Njombe. Mgombea ubunge
wa jimbo la Wanging'ombe kupitia CCM Dkt. Festo Dugange ameahidi kuwa endapo
atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakilisha anaweka mazingira mazuri ya
wawekezaji kujenga vyuo katika jimbo hilo.
Hayo ameyasema kwenye
uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Wangingombe uliofanyika kata
ya Wanging'ombe kijiji cha Wanging'ombe wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe.
Alisema iwapo atakuwa
mbunge wa jimbo hilo atavutia wawekezaji wa serikali na hata binafsi ili waweze
kujenga vyuo katika jimbo hilo ili kuongeza tija kwa wanafunzi wanaomaliza
kidato cha nne na cha sita.
Alisema chuo hicho
kitakapojengwa kitatoa nafasi kwa wanafunzi kujiendeleza katika fani mbali
mbali ili waweze kupata ujuzi ambao utawasaidia katika kuendesha shughuli zao
za kimaisha.
Alisema chuo hicho pia
kitawawezesha wananchi wote hasa vijana ambao watakuwa tayari kufanya biashara
waweze kufanya hivyo ili nao waongeze kipato chao na cha familia kwa ujumla.
"Tukifanya hivyo
tutawezesha halmashauri ya Wanging'ombe kupatamapato ya kuhudumia jimbo letu
hii kutokana na muingiliano wa watu utakavyokuwa baada ya kujengwa kwa
vyuo" Alisema Dkt. Dugange.
Nae mwenyekiti wa CCM
wilaya ya Wanging'ombe Stephano Kinyangazi alisema jimbo hilo limepewa heshima
kubwa ya kutoa viongozi wa kitaifa hivyo wananchi wanapaswa
kujivunia na kuiendeleza kwa kuchagua viongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi.
"Makamu
mwenyekiti, naibu katibu mkuu na katibu wa itikadi na uenezi ngazi ya taifa wote
wanatoka Wanging'ombe hivyo tusiwaangushe hawa vingozi tuchague diwani, mbunge
na raisi kutoka CCM" Alisema Kinyangazi.
Wananchi walioshiriki
kwenye uzinduzi wa kampeni akiwemo
Rehema Ngoda na Elias Mwanzela walisema endapo kutajengwa vyuo katika jimbo la
Wanging'ombe itakuwa faraja kwao kwani watoto wao watakuwa wanasoma
karibu tofauti na sasa ambapo wamekuwa wakienda kusoma vyuo vilivyopo mbali na
maeneo yao.
"Namshukuru
mgombea kwani jambo la chuo litatukomboa kwenye jimbo la Wanging'ombe kwasababu
mpaka sasa hatujawahi kuwa na chuo kinachotambulika kiserikali vipo vyuo
vingine tu vya kanisa lakini kwa chuo cha serikali hatuna" Alisema Elias.
"Sisi wakazi wa
kata ya Wanging'ombe hatuna chuo hivyo endapo kitajengwa tutafurahi watakuwa watusaidia
kwani hali yet ya kiuchumi inatufanya tushindwe kuwapeleka watoto vyuoni kwa
kuwa ni gharama kubwa"


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...