Na Mwandishi wetu, Babati
MTUMISHI
wa Baraza la ardhi na nyumba Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Ruth
Semkuyu amefikishwa kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya
hiyo kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya shilingi 100,000 kwa ajili
ya kukazia hukumu.
Semkuyu
alifikishwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kwenye
mahakama hiyo jana mjini Babati mbele ya hakimu Simon Kobelo.
Mwendesha
mashtaka wa TAKUKURU Evelyine Onditi akisoma hati ya mashtaka ya kesi
hiyo ya jinai namba 155/2020 amesema Semkuyu ametenda kosa hilo akiwa
ofisini kwake mjini Babati.
Onditi
amesema Semkuyu akiwa kwenye ofisi ya baraza la ardhi na nyumba Wilaya
ya Babati aliomba rushwa kwa mkazi wa eneo hilo ili kukaza hukumu baada
ya kushinda kesi yake kwenye baraza la kata.
Amesema
Semkuyu alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
Hata
hivyo, Semkuyu alikana shtaka hilo mahakamani hapo alipoulizwa na
Hakimu Kobelo kama ni kweli ametenda kosa hilo la kuomba na kupokea
rushwa ya shilingi laki moja.
Mshtakiwa
huyo amepelekwa rumande kwenye gereza la mkoa huo la Mrara, mara baada
ya kushindwa kutimiza masharti ya kupata dhamana.
Hakimu Kobelo anayeshikilia kesi hiyo ameahirisha hadi Septemba 23 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...