Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini Ummy Mwalimu amesema endapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Tanga Mjini atahakikisha Uchumi wa Jiji hilo unaamka upya kurudi enzi zake.
Ummy akizungumza katika mkutano wa Kampeni kata ya Nguvumali amesema kipaumbele chake kikubwa ni kufufua Uchumi wa Tanga kwakusukuma Ujenzi wa Viwanda vipya na kufufua vile vilivyokufa, Maboresho ya Bandari Awamu ya pili,Kusukuma Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima-Chongoleani na kusimamia uwezeshaji Kiuchumi kwa akinamama na vijana.
Kukamilika kwa mipango hiyo kutazalisha ajira nyingi za mojakwamoja na kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi na kufanya ustawi wao kiuchumi kuwa imara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...