Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MGOMBEA
ubunge wa jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, kwa tiketi ya CCM
Christopher Ole Sendeka (Simba wa Manyara) amesema kero ya wadau wa madini ya Tanzanite wa
Mji mdogo wa Mirerani kupanga foleni ili wapite kwenye lango la ukuta
unaozunguka migodi ya madini hayo pindi walitoka ndani inapaswa kupatiwa
ufumbuzi.
Ole Sendeka
ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa CCM mji mdogo wa
Mirerani ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Amesema
wadau wa madini ya Tanzanite wanakuwa na wakati mgumu pindi wakitoka
migodini kwani kuna maeneo mawili pekee ya kukaguliwa.
Amesema kuwa watu zaidi ya elfu 10 kuwa na sehemu mbili pekee za wanaume na wanawake kupekuliwa kwa siku moja hazitoshi.
"Tunaomba
mheshimiwa Waziri Mkuu ufikishe salamu zetu kwa Rais John Magufuli juu
ya ombi letu la kutuongezea sehemu ya upekuzi," amesema Ole Sendeka.
Amesema endapo maeneo ya upekuzi yakiongezwa wadau watafanyiwa upekuzi kisha wataondoka mapema kurudi majumbani mwao.
Amesema
wakati mwingine mistari miwili ya kupekuliwa inakuwa mirefu hivyo wadau
wa madini husimama kwa muda mwingi kusubiri kupekuliwa.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema anachukua suala hilo na
kukifikisha kwa Rais Magufuli ili waweze kuona jambo la kufanya.
"Ninyi
cha kufanya ni kuhakikisha mgombea wetu Rais Magufuli anapata kura
nyingi za kishindo kwa maslahi mapana ya wananchi ili kushughulikia
hilo," amesema Majaliwa.
Mgombea
udiwani wa Kata ya Endiamtu, Lucas Chimbason Zacharia, amewaomba
wananchi wa eneo hilo kumpa kura nyingi za ndiyo ili ashike nafasi
hiyo.
"Kwa pamoja
tutafanikiwa kufanikisha maendeleo yetu sisi wananchi hivyo tusifanye
makosa Oktoba 28 mwaka huu katika kupiga kura," amesema.
Mgombea
ubunge wa Jimbo la Simanjiro Mkoani Manyara, Christopher Ole Sendeka
(Simba wa Manyara) akiomba kura kwa wananchi wa Kijiji cha Landanai, Kata ya Naberera,
kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo
mhandisi Zephania Chaula.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...