MKUU Wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa wito Kwa wanawake nchini kujiamini na kuonyesha uwezo wao kwenye nafasi mbalimbali wanazopatiwa ili waweze kufanikiwa katika kila jambo.

RC Kunenge ameyasema hayo wakati Wa ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha Viongozi wa Dini, Wanasiasa na Watetezi wa haki za wanawake uliolenga kuhamasisha amani na haki ambapo amesema anaamini wanawake wanao uwezo Mkubwa wa kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii hivyo amewataka kutumia vizuri nafasi zao.

Aidha RC Kunenge amesema serikali ya Mkoa wa Dar es salaam itaendelea kulinda na kuweka mazingira mazuri ya kuhakikisha haki ya kila mmoja inalindwa na kuheshimiwa Kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kulinda amani, utulivu na upendo Kwa mustakabali Wa maendeleo na kuwakumbusha kuhudhuria mikutano ya kampeni ili waweze kupima sera za wagombea.

Mkutano huo wa kuhamasisha amani na haki umeandaliwa na chama cha wanahabari Wanawake Tanzania TAMWA Kwa kushirikiana na taasisi ya Amani Tanzania ambapo tayari mikutano ya aina hiyo imeshafanyika kwenye kanda za Arusha, Dar es salaam, Dodoma na Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...