MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akizungumza wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya majikujionea namna unavyotekelezwa eneo la Horohoro Mkinga mkoani Tanga ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais DktMagufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribuzaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani kushoto ni Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akifuatiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo akizungumza wakati wa ziara hiyo

Mkurugenziwa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akieleza jambo wakati wa ziara hiyo kuhusu mradi huo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga MartineShigella

Mkurugenziwa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akimpokea Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati alipofanya ziara kwenye mradi wa maji waHorohoro

Mkurugenziwa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo
Mkurugenziwa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella katika wakati alipotembelea mradi huo kulia ni Mhandisi Upendo Lugongo anayefuatia kwa nyuma ni Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga Joseph Sura

MKUUwa Mkoa wa Tanga Martine Shigela ameitaka Mamlaka ya Maji Safi,Usafi waMazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili yakuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji la Hohorohorowilayani Mkinga.

Shigelaaliyasema hayo leo wakati alipofanya ziara yake ya kutembelea miradi ya maji kujionea namna unavyotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribuzaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani

Ambapomradi huo unatekelezwa na Mamlaka Tanga Uwasa una thamani ya milioni 360 upo kwenye asilimia85 na mmehaidi asilimia 15 zilizobakia mtakamilisha ifikapo mwisho wa mwezi Septemba mwakani

“Ndugu zangu Tanga Uwasa mnafanya kazi nzuri sana lakini hakikisheni mnatenga fedhakwa ajili ya kuimarisha maeneo yanayotorosha maji kwenye bwawa la maji laHohorohoro wilayani Mkinga”Alisema

“Lakini pia Bwawa hili kwa kweli halitoshelezi kama mnavyoona maji yamepungua sana nimeelezwa kupitia fedha mlizonazo za PFR mhakikishe mnatenga fedha kwa ajili yakuimarisha maeneo yanayotorosha maji”Alisema

Hata hivyo aliwataka pia kuanza upanuzi wa bwawa hilo kupitia force akaunti ili mvuazitakaponyesha wawe na uhakika wa kuhifadhi maji huku akieleza umuhimu wakuhakikisha wanaongeza vilula vya kuchotea maji wananchi kutokana na kwambahivi sasa vipo vichache ili kuwaepusha kujazana eneo moja.

“Nizipongeze mamlaka za Maji Mkoa wa Tanga kwa kuona umuhimu wa kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Rais Dkt Magufuli ya kuona namna serikali yake inawafikishia maji wananchi kwa ukaribu zaidi na kutekelezwa kwa vitendo kauli mbiu ya kumtua mama ndoo kichwani”Alisema RC Shigela.

Hata hivyo alionyeshwa kufurahishwa na hatua ya mradi huo ilipofikiwa huku akihaidikwenda kukagua kuona kama maji yanatoka Octoba 15 kuja kuona kama maji yanatokaeneo hilo la Horohoro.

“Kwa sababu eneo la Horohoro kwetu sisi ni eneo la kimkakati kwa sababu tunataka iwendio iwe habu ya biashara kati ya Kenya na Tanzania watu wanaotaka kufanya biasharawafike eneo hilo watapata bidhaa kutoka Kenya na Tanzania”Alisema
 
Awaliakizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hillyalisema Tanga Uwasa wanajenga mradi huo kwa kushirikiana na Ruwasa na umefikiaasilimia 85.

MhandisiHilly alisema wanategemea mpaka ifikapo ndani ya mwezi wa Septemba na Octoba kaziza msingi zitakuwa zimekamilika na wananchi kuendelea kuhudumiwa kama ilivyopangwatangu mwazo pamoja na na kituo cha Forodha cha Horohoro mpakani.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema mradi huo utakamilika kwa muda uliopangwa kwa mwisho wa mwezi waSeptemba mwaka huu watu waanze kunywa maji lakini kwa maboresho ambayoaliwaagiza kuyafanya watahakikisha yanafanyika kwa fedha kidogo walizopokea.

Alisema ili wananchi wanapata maji safi na salama ikiwemo kuhakikisha bwawa hilo linauwezomkubwa wa kutunza maji kwa kufanyia maboresho kwenye maeneo yaliyoonekana nachangamoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...