Charles James, Michuzi TV

SERIKALI kupitia wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano sekta ya mawasiliano Nchini imetoa rai kwa watendaji wa taasisi ya umma ya Posta iliyopo chini ya sekta ya mawasiliano kufanya kazi kwa matokeo makubwa lengo likiwa kuinua shirika hilo kwa kufanya mabadiliko ambayo wananchi watayafuraia.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu mtendaji sekta ya mawasiliano, Dk Zainab Chaula wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha semina elekezi ya mafunzo ya uongozi na utendaji kwa watumishi wa taasisi ya serikali Posta Nchini. 

“ Kwanza tufanye kazi kwa bidii’ maana yake ni matokeo, matokeo ni kuhudumia jamii kwa kutengeneza fursa za ajira na fursa za kiuchumi na msisahau tayari tumeingia kwenye uchumi wa kati hivyo kwa miaka mitano ijayo lazima twende kwenye uchumi wa kati wa juu” Amesema Chaula.

Aidha ameongeza kuwa Tanzania ya sasa ni Nchi ya kidijitali kutokana na kuwepo kwa matumizi ya mifumo mbalimbali inayotumika katika Maisha yetu ya kila siku ikiwemo matumizi ya habari, anuani za makazi kwa ujumla wake Posta kiganjani mwako.

Kwa upande wake Posta master mkuu mkoa wa Dodoma, Hassan Mwang’ombe akaeleza baadhi ya huduma ambazo taasisi hiyo imekuwa ikizitoa ambapo moja ya huduma hizo ni Pamoja na uwepo wa huduma mama yaani EMS, huduma za barua, huduma ya barua za kawaida na huduma za fedha.

Pia huduma zingine ni biashara ya mtandao BICOM, huduma ya kubadili fedha za kigeni, ukusanyaji wa maduhuli, huduma ya photocopy, huduma za kibenki, malipo mbalimbali ya serikali Pamoja na huduma za uwakala ambazo tayari zimewafikia wadau mbalimbali ikiwemo baraza la mitihani NECTA, TCU, NMB, CRDB, HAZINA, TPB na TANESCO.

Mafunzo hayo yamefunguliwa rasmi tarehe 14 ya mwezi wa tisa 2020, ambapo yanatarijiwa kudumu kwa muda wa siku tano lengo kuu likiwa ni kuhakikisha taasisi ya serikali ya POSTA inaleta mabadiliko katika kuhakikisha huduma zake zinakua zenye tija na manufaa kwa wananchi ili jamii iweze kutambua na kutumia mfumo huo kikamilifu.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk Zainab Chaula akizungumza na watumishi wa Posta kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha semina ya mafunzo kwa watumishi wa serikali POSTA. mafunzo yenye lengo la kujadili masuala ya uongozi na utendaji kazi mahala pa kazi.
 Posta Master Mkuu, Hassan Mwang'ombe akizungumza na washiriki kutoka mikoa mbalimbali wa Shirika la POSTA Nchini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha semina ya mafunzo ya siku tano jijini dodoma.
 Washiriki wa taasisi ya serikali ya Umma POSTA wakiwa kwenye kikao kazi cha ufunguzi wa semina ya mafunzo ya utendaji na uongozi yanayofanyika kwa siku tano jijini dodoma ambayo yamezinduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Zainab Chaula.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...