Jane Edward,Arusha
Serikali imeendelea na usambazaji wa huduma za umeme mijini na vijiini ambapo kwa wilaya ya Monduli uunganishwaji wa umeme ni asilimia 45,huku kwa Mkoa mzima wa Arusha ni asilimia 77.
Akizindua uwashaji wa umeme katika zahanati ya Kijiji cha Lendikinya na kwa baadhi ya nyumba ambazo zipo kwenye mradi wa umeme wa Rea awamu ya Tatu, Naibu Kamishna wa Nishati kutoka wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luhoga amesema utekelezaji wa mradi huo ni maagizo ya Waziri wa Nishati Dr Medard Kalemani ambaye alifanya ziara katika Kijiji hicho na kubaini kusuasua kwa mkandarasi aliyekua akitekeleza mradi huo hali iliyopelekea kumfukuza kazi na kumpa mradi huo Tanesco Mkoa wa Arusha kuutekeleza.
Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Monduli ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Monduli Robert Syantemi akizungumza na wananchi waliojitokeza katika zoezi la uwashaji wa umeme tayari amewataka wananchi kutumia fursa zinazotokana na Nishati hiyo katika kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo ikiwemo kuyaongezea thamani, na kubuni miradi midogo midogo ili kupata kipato.
Aidha ameitaka Tanesco kuongeza utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi vijiini na kufuata maagizo yote yanayotolewa na viongozi ngazi za juu pamoja na kuziainisha changamoto zinazokwamisha miradi hiyo kwa wakati ili Serikali iweze kuzitatua kwa Wakati na hatimaye wananchi wote kuweza kunufaika na umeme.
Kwa upande wao wanufaika wa umeme huo wameishukuru Serikali ya Awamu ya tano kupitia shirika la umeme Tanzania Tanesco kwa kuweza kuleta Mwanga katika kijiji hiko kwani awali Kijiji hicho kilikuwa na giza .
Hata hivyo Hadi sasa umeme kwa nchi nzima ni vijiji elfu 12, 268 ambapo kwasasa tayari vijiji 9600 vimekwishafikiwa na umeme wa Rea uku vijiji takriban 2600 vinatarajiwa vitakamilika 2021 .
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Monduli Robert Syantemi, akikata utepe kuashiria uwashwaji wa umeme Katika kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Arusha injinia Herin Mhina akizungumza na wananchi katika hafla ya uwashwaji umeme
Naibu Kamishna wa Nishati ya umeme nchini injinia Innocent Luoga akizungumza na wanakijiji Katika Kijiji cha Lendikinya wilayani Monduli
Picha ya pamoja
Kamishna wa umeme akionyesha namna umeme unavyowaka







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...